Nasema haiwezekani. Nina uzoefu mkubwa kikazi na tbl, nbcl (coke). Naamini hata sbl hali ni hiyo.
Kwa wingi huo naamini unajipanga kuwa wakala.
Kuna taratibu unapaswa kuzifuata kabla ya huo uwakala na lazima waje kukukagua eneo la kazi, stoo, wafanyakazi, vitendea kazi km magari madogo ya kusambazia wateja (diliveries kwa wateja km baa, grocery nk)
Minimum capital kwa miaka niliyokuwa nafanya kazi ilikuwa 200,000m na hiyo inakuwa fixed kiwandani sio ya kuombea oda. Maana yake kutoa oda ya gari moja ilikuwa km 65m, hii ni tofauti na hizo.
Kumbuka ni dhamana yako siku kikitokea chochote kikaathiri biashara na yumkini vitendea kazi vya kampuni wana-seize hiyo fixed.
Hizo 1,000 cases utapata kwa wakala jirani.wanagawa uwakala kwa utaratibu maalum ili kuepuka kuingiliana kimaslahi au hadi wakala mzoefu awe ameonesha kuelemewa au anakiuka masharti.
Kukiuka masharti ya mkataba wao kunatosha kukufutia uwakala na kusimamisha huduma.
Mtafute wakala jirani au dealer wa tbl/maafisa masoko.
Tbl hawana kona kona km waswahili. Maboss ni makabulu na head ofisi iko dar na SA ndio kitovu cha yote kuanzia utawala na control ya magari nk. Itoshe kusema wako smart na wanajiamini na biashara zao. Hawababaishwi na kupoteza mteja msumbufu.