Nawezaje kufuta nafasi moja kati ya nilizoomba UTUMISHI?

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
13,966
Reaction score
26,220
Nimefanya applications hizi nafasi mpya za TRA, nimeapply nafasi mbili ila utumishi wamesema tuombe nafasi moja tu hata kama mtu unaqualify zote. So nataka kuifuta nafasi moja ya Tax Management Officer ii na nibakishe custom officer ii pekee.

Naombeni msaada nikiziacha zote mbili kutakua na madhara,na je nikitaka kuifuta hiyo moja inayizidi nifanyaje?

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
 
Weka hilo tangazo hapa

Kama huwezi kuliweka tukuelekeze wacha tukose wote
 
Sidhani kama ina madhara sana.watakuchagulia moja wenyewe au watakuchagua zote wewe mwenyewe uamue uchague ipi ya kufanya.sema wakikuchagulia wenyewe wanaweza kukuchagulia hiyo usiyoitaka.so kukushauri unaweza kuwapigia wenyewe au kuwatembelea ofisini kwao wakusaidie kuifuta au unaweza kufanya kama una edit hiyo usiyoitaka halafu utaattach kitu kingine kisichohusiana na barua ili wakati wa screening wakiangalia eneo la barua yako wakute umeattach kitu kingine hence watakudisqualify kwenye hiyo nafasi na moja kwa moja watakuchagua kwenye hiyo unayoitaka.
 
Acha uoga watakuchagua moja tu jina lako likisoma kwenye system halijirudii mara mbili.
 
Kuifuta mwenyewe haiwezekan ila cha msingi unaweza kufanya kama una edit hiyo usiyoitaka then sehemu ya barua unaweka kitu chochote kisichohusiana na barua.

Wakija kukagua attachments watakuta hujaweka barua.automatically wanakupiga chini kwenye hiyo post.

Otherwise tembelea ofisi zao Dodoma.
 
Piga simu mzee

Sent from my TECNO CC6 using JamiiForums mobile app
 
Skia mkuu, asije mtu akakufariji kuhusu hili, you know utumishi wako very serious na mambo Yao kama tangazo lishasema kuwa Omba nafasi moja hata kama umequalify zote basi fanya hvyo kwa maana hizo nafasi zote ziko taasisi zmoja, kitendo Cha kuomba nafasi zote utakuwa umeenda against na sheria zao na utakuwa umejidisqualify.. hapo fanya Kila namna ubaki on one position.
Narudia tena utumishi si watu wa mchezomchezo.

Halafu mkuu kwa nn umeomba zote Hali ya kuwa wameshatangaza mtu aombe moja tu.. huoni kama umejitekenya mwenyewe, na ubaya wa portal Yao ukiomba zote hata haikatai Ila kwenye shortlisted utakiona Cha mtemakuni.
Hata usipocertify vyeti unaweza kutuma maombi freshy tu ila kwenye shortlisted....
 
Yani hapo apambane ibaki 1 utumishi siku hizi wapo serious mno hawatomwita hata 1
 
Naona sasa umeshakua na adabu maana ulikuaga mbishi sana kwny inshu ya ku-certify vyeti.Naona walikunyoosha mzee.
 
Daah Mzee usinikumbushe machungu, yaan tulibishabisha hapa kumbe kiama ndo kilikuwa kinanijia.. Sasa hv nimecertify Hadi cheti changu Cha ndoa kudadeq navyote nimeweka.
Utumishi sio poA
Naona sasa umeshakua na adabu maana ulikuaga mbishi sana kwny inshu ya ku-certify vyeti.Naona walikunyoosha mzee.
 
Yani hapo apambane ibaki 1 utumishi siku hizi wapo serious mno hawatomwita hata 1
Wale watu ni hatari, tena kama umeangalia vizuri kwenye hili tangazo lao la Sasa hayo maneno wameweka bold yaan kuonesha msisitizo, yaan mshikaji asijichanganye, mda anao na afanye Kila namna hiyo received moja iondoke.
Hapa wadau wanamwambia sijui atoe barua mara aweke kitu kingine hyo haitosaidia kosa ni kosa tu, awapandie Ofisini hukohuko kabla window halijawa closed
 
Sikua nimeona hicho kipengele cha kuomba nafasi moja tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…