inawezekana kabisa ila mpaka uwe na sababu, mfano mimi kuna kipindi nilipataga vihela nikapambana sana kusaidia ndugu zangu kwa kadiri nilivyoweza, nakumbuka nikapataga kesi central police nilikaa pale kama wiki mbili ndugu karibu wote walipata taarifa lakini hakuna lolote walifanya kunisaidia nilijipambania mwenyewe nikatoka , baada ya kutoka maisha yangu yakawa magumu sana , ila sikukata tamaa ndo bdae hali ikawa poa, nikaona wamenza kujirudi so kuanzia hapo nilisema sina ndugu niko mwenyewe duniani, hta leo nikumwa ni mimi na Mungu wangu, yaani moyo wangu usharidhika kbs, napambana mwenyewe, basi