Nawezaje kuishtaki kampuni ya simu?

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Kuna mchezo nimegundua kuwa nafanyiwa na Kampuni fulani ya simu kwa kunikata pesa zangu bila ridhaa yangu ile airtime, ukiwapigia wanasema kuwa ulijiunga na huduma hizi. Nimewalalamikia mara nyingi sana ila wameendelea kunikata tu. Kila ukiwaambia wanakuambia jitoe, najitoa lakini baada ya muda unakuta unakatwa tena.

Wasi wasi wangu ni Watanzania wangapi ambao huenda wanakatwa bila ridhaa yao na bila wao kufahamu? Maana hadi uwe makini ndio utagundua kuwa wanakukata! Nikipata ushauri mzuri na mwana sheria anayeweza kunisimamia katika hili nitashukuru sana ili haki itendeke.
 
Bila shaka hao ni tigo,

Cha msingi nenda customer centre yao, Waambie wakufute kweye huduma zote za kijinga jinga
 
Bila shaka hao ni tigo,

Cha msingi nenda customer centre yao, Waambie wakufute kweye huduma zote za kijinga jinga
Mpwa naomba nisikubali au kukataa kuwa ni Tigo au lah ila nimeshwapigia mara nyingi sana, wanachokifanya ni kwamba leo wanakutoa baada ya week unashtuka unakuta salio limepungua ukifuatailia unakuta wanakukata, unawasiliana nao tena inakua the same same story. Yaani ninachoomba hapa ni namna tu ya kuwashtaki, staki tena.
 
Ndo mchezo wao mimi voda kila nikiweka vocha wanakata sh 42..yani nimewapigia wanadai sikatwi. Natafuta muda nawaibukia alafu napiga hesabu 42 mara siku nilizokatwa
 
Ndo mchezo wao mimi voda kila nikiweka vocha wanakata sh 42..yani nimewapigia wanadai sikatwi. Natafuta muda nawaibukia alafu napiga hesabu 42 mara siku nilizokatwa
Kulikua na Uzi wa tpaul nimeutafuta sijauona alikua akielezea wizi unaofanywa na haya makampuni aiseeee. Hivi bado TCRA wako humu ndani??
 
mkuu, kabla ya kuwanyoosha inabidi kwanza uende kwao physically uwaombe wakutoe kwenye huduma hiyo na ikibidi uwarekodi kwa siri kama ushahidi...kama bado wataendelea kukukata, ukipata wakili mzuri kama Tundu Lissu atawanyoosha hawatakuja kusahau.
 
Kumbe huu mchezo sio wa leo wala wa Jana eeghhh, na mimi nimeambiwa hivyo hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…