Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Kuna mchezo nimegundua kuwa nafanyiwa na Kampuni fulani ya simu kwa kunikata pesa zangu bila ridhaa yangu ile airtime, ukiwapigia wanasema kuwa ulijiunga na huduma hizi. Nimewalalamikia mara nyingi sana ila wameendelea kunikata tu. Kila ukiwaambia wanakuambia jitoe, najitoa lakini baada ya muda unakuta unakatwa tena.
Wasi wasi wangu ni Watanzania wangapi ambao huenda wanakatwa bila ridhaa yao na bila wao kufahamu? Maana hadi uwe makini ndio utagundua kuwa wanakukata! Nikipata ushauri mzuri na mwana sheria anayeweza kunisimamia katika hili nitashukuru sana ili haki itendeke.