Nawezaje kujua au kutathimini ili kujua bei halisi ya kiwanja

Nawezaje kujua au kutathimini ili kujua bei halisi ya kiwanja

renamaizo

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2014
Posts
2,134
Reaction score
3,064
Habar wadau hope wote mpo poa

Maisha magumu lakini elimu pia inasaidia ila yenyewe bila ujanja ni kazi bure ujanja muhimu pia ukiongezea na elimu basi ni full mteremko !!!! nije moja kwa moja kwenye mada naomba ijulikane wazi hapa tunazungumzia bei au thamani ya kiwanja na sio nyaraka utapeli au upimaji wa viwanja na kupata hati NOOOOOOO TUONGELEE BEI

Mi ninavyojua bei ya kiwanja inaevalutiwa kutukana na 1 sqm Hiii ndio unit measurement it means km 1 sqm = 10000 TZS basi liwamja chenye ukubwa wa 200 sqm = 200000 TZS

kwaio thamani halisi ya uwanja inatokana na ukubwa wake

Lakini io 1 sqm price sijui utaevaluate vipi??????
Lakini uzuri wake oarameters zipo zipo na tena itakuwa poa tukaweka zile za muhimu from top to bottom

Parameters hizo ni km
1. Location ; kipo city centre au ni uko ndani ndani mbagala charambe viwanja vilivo city centre ni bei Weee
2. Distance from city centre
3. Topography flat au mlima
4. Land use
6. Others

sasa kichekesho kinakuja unaenda mahali kununua kiwanja unakuta mtu ana kiwanja kimoja kakigawa sehemu nne kila kimoja kina 100 sqm kila kioja anauza million 3 na hati hana kipo ndani ndani huko majoe viwege na hti hana hii imekaaje afu kibaya zaidi wakikupeleka wanaanza kukuforce ununue haraka kwa madai kuwa ukichelewa kuna mtu atakinunua fasta

Naombeni ushauri wapi naweza pata wataalamu wa kutathimini bei za viwanja

Nisije kununua baadae kuja kushtuka nimepigwa
 
Inategemea na mahali kilipo pamoja na miundo mbinu iliyopo; muhimu nafsi yako iridhie kutokana na mazingira
 
Kuwa makini matapeli ni wengi hadi huku jf wapo.
Kwa hali ya kawaida thamani ya kiwanja hutokana na eneo lilipo, fursa zilizopo, uhitaji, upatikanaji mengine watajazia wachangiaji wengine
 
Kuwa makini matapeli ni wengi hadi huku jf wapo.
Kwa hali ya kawaida thamani ya kiwanja hutokana na eneo lilipo, fursa zilizopo, uhitaji, upatikanaji mengine watajazia wachangiaji wengine
nan atafanya evaluation uswahili mwingi sana unakuta mtu kiwanja sio chake nae anashupqliq ununue ananufaika vp
 
nan atafanya evaluation uswahili mwingi sana unakuta mtu kiwanja sio chake nae anashupqliq ununue ananufaika vp
Tuachane na uswahili, umeshachunguza n vipi wenzetu wanafanyaje? Reference ni nzuri
 
wapi naweza pata wataalamu wa
tuachane na uswahili, umeshachunguza n vipi wenzetu wanafanyaje? Reference ni nzuri
subor wajuz waje ? maana me kupanga bei kisela hapana nilishalizwa miaka fulani hv kitu unauziwa million 3 na kumbe hapo nyuma kuna mwingine kauziwa million 1.9 ukilalqmika wanakuambia hii ni biashara ela hazirudishwi
 
mkuu valuation ya bei ya kiwanja unaweza kufanya kwa kutumia registered valuers - hawa wapo wa Gov na private na ofisi zao zipo kila mkoa/wilaya. Pia unaweza kutumia uzoefu kukadiria thamani ya kiwanja - hii unaipata kwa kusoma bei za viwanja kwenye watsup, twitter, zoomtanzania, magazeti&majarida,etc. Hii ya uzoefu ndio unapata kujua mfano maeneo ya mbweni sqmtr inaanzia tshs laki moja; kigamboni elfu 10 hadi 15 per sqmtr, etc.

Ila njia zote bado mwisho wa siku zinakuwa determined na kiasi cha pesa ulichonacho eg kama una 10m usiogope ukisikia kiwanja kinauzwa 25m unaweza kabisa ukashusha bei hadi hiyo 10m uliyonayo. Muhimu usiwe na haraka wala kuyumbishwa na maneno ya madalali, wapambe na wauzaji.
 
100sqm ( 10mx10m) unajenga nn sasa hapo duka ama?
 
Kiwanja kipo king’azi kinyerezi malamba, hatua 20 kwa 25 Bei 8 million piga simu 0693300971
 
Back
Top Bottom