sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Napenda sana wanyama, kwangu ni viumbe wenzetu tulioumbwa nao pamoja isipokuwa sisi tulipewa upendeleo mkubwa wa kuwa na akili na kupewa mamlaka juu yao. Hata nyumbani kwangu nawajali sana wanyama, hata kuku nikimleta kwajili ya kitoweo basi haki yake ya mchele, maji na banda safi ataipata.
Ipo hivi, kuna sehemu huwa tunaenda kukagua maendeleo ya mradi flani, n.k. kwa wiki tunaenda kama mara 3 hivi.
Sasa hio sehemu nilimkuta paka, hana mtu rasmi wa kumlisha, huwa anapambana kivyake, kuna kipindi namuona kabisa hajala anahangaika kutafuta msosi, hali hii mbele ya macho yangu ilikuwa inanipa majonzi.
Basi nikaanza mazoea ya kujifanya najinunulia samaki wa kula mchana sehemu ya karibu, ila nilikuwa naenda kisehemu flani hivi kimejificha nampa huyo paka anakula..
Nikiona kuna watu hio sehemu navyompa samaki, inakuwa bahati mbaya kwake maana siwezi kumlisha waziwazi, watu wataanza kunitilia mashaka
Sasa paka amekuwa akinizoea sana, yani kila nikienda nikishuka tu huyo anakuja miguuni anaanza kulia meow, meow, meouw! Kujizungusha zungusha, napenda lakini hii huwa inawajenga watu picha mbaya juu yangu kwahiyo inabidi nimfukuze tokaa!! Japo lazima ntamlisha kwa usiri.
Sasa kuna siku katika maongezi ya hapa na pale, raia flani akaanza story kwamba nimezoeana sana na paka na sio vizuri kuzoeana nao, nikijaza deshi hapo ni mambo ya kishirikina.
Nifenyeje huyu paka aache mazoea.