sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Mtaani kwangu kuna kijana yupo hapa kwa miezi miwili, yupo kwenye rika la miaka 24 hivi, ana frem anauza mahitaji ya nyumbani na vilevi, lakini biashara yake kuu yenye wateja wengi ni Bangi ambayo wanunuzi huvuta hapo hapo ama maeneo ya karibu, eneo sio la barabarani, huwa kuna watu wachche wanatumia hii njia.
Ni kijana mjanja mjanja, nilienda siku moja hapo kumcheki, kiukweli ana kipaji kikubwa sana cha kutengeneza urafiki, ndani ya dakika 4 tu tushazoeana na matani ya hapa na pale maana mimi pia nipo miaka 31 so ni kijana mwenzangu.
Sina tatizo na dogo ila ni hawa wavuta bangi, wengi hawana shughuli za kuwaingizia vipato, wakivuta bangi wanasizi tu, Pia bangi wanazovuta ni haya makapi ya shilingi 500 yanayouzwa karibu kila kona ya nchi, sasa hawa vijana kama hawajishughulishi na wanapenda bangi kinachofuata huwa ni wizi / utapeli, pia hatari kubwa ipo kwa ma house girl tunaowaachia nyumba zetu tukiondoka, wanaweza kurubuniwa na hawa vijana kirahisi.
Nyumba zipo 9 kwenye huu mtaa na zote zina fensi na mageti lakini kuna matukio kadhaa yamewahi kutokea watu kuibiwa nguo, tv, n.k. japo ni nadra, hatutaki yajirudie mara kwa mara.
Sasa ili kutatua matatizo hayo kabla hayajatokea mimi nimeona nishughulike haraka, ila kwa sharti moja tu, sitaki kushirikisha mkono wa sheria kwa sababu dogo anaweza kuishia mahabusu kesi yake ikasikilizwa 2040 na akienda mahakamani ni miaka 30 jela. Kinachonifanya nikwepe kutumia sheria ni hayo maisha ya Jela na Mahabusu kwa huku bongo, asikwambie mtu hizo sehemu hazifai hata kidogo, sikiaga tu flani yupo huko, sio kuzuri hata chembe.
Niliwahi kumwambia hio ishu itamuharibia life lakini dogo yeye anasema hakuna pusha asiejua hatari ya biashara anayofanya, anasema hajaingia kichwa kichwa anajua anachokifanya, kiufupi anajiamini sana lakini haiondoi uhalisia kwamba bado yupo hatarini.
Kijana ana miaka 24, haitakuwa vema mimi nihusike kwa yeye kutoka jela akiwa kamalizia ujana nyuma ya nondo.
Ni vipi nitaweza kutatua hili tatizo bila kushirikisa polisi.