Nawezaje kumtoa pusha wa mtaani bila kutumia Polisi, sitaki dhambi ya kumfanya mtu atoke jela akiwa mzee

Nawezaje kumtoa pusha wa mtaani bila kutumia Polisi, sitaki dhambi ya kumfanya mtu atoke jela akiwa mzee

Weka fence ya umeme kwako, hao mapusha hawatasogelea kwako.

Kifupi ni kwamba wewe imarisha ulinzi wa nyumbani kwako tuu basiii, mengine achana nayo.
Hatari i kubwa sana, hata watu wanaopita kwa miguu hapa wataanza kukabwa, pia hata ma house girl wanweza kurubuniwa na hawa watu wakatuvamia usiku maana wengi hawana shughuli za vipato na wanapenda bangi sana, mvuta bangi akiwa na kiu (arosto) ni hatari sana
 
Muelekeze tu kuwa biashara yake inaharibu vijana akili na kupelekea wao kufanya uhalifu hivyo yeye kama ataweza aachane nayo kama hawezi kuiacha basi wakae washauriane na wateja wake juu ya kuacha vitendo vya uhalifu mtaani na kama itatokea uhalifu wowote na ulishawaonya basi hatua kali zitachukuliwa, In piece tu ili baadae usije niweka kwenye history of your life kuwa ni part ya kuyaharibu.
 
Mkuu hizo bangi mimi sio mgeni..... ni mstaafu

Hivi kwa akili yako unadhani haya makapi ya jero (shilingi 500) ndio bangi wanazovuta marekani ama ulaya??

Huku kwetu tunalima bangi nzuri sana yenye kiwango cha juu ila sasa wakulima wenyewe wanawahi kuvuna bangi mbichi kuogopa kukamatwa, bangi wakipanda hawazihudumii kutoa wadudu wanaoharibu maua, hawatoi vifundo vilivyooza, n.k. nae pusha ni mweupe tu yeye anachojua ni kusambaza tu, anaangalia kama imetoka mkoa unaosifiwa, hata akipewa ambayo haijakomaa ama ambayo imevunwa miezi mitatu iliyopita ananunua hivyo hivyo tu, huku kwa wateja ndio awaonea huruma maana waavuta uchafu wa 500 wakidhani wanavutakitu chenyewe, matokeo yake ndio haya wengine vichwa vinauma, macho yanakuwa mekundu kuzidi kiwango cha kawaida cha bangi halisi, wengine wanakuwa vichaa kabisa.

Unaeza kusoma uzi wangu huu wa elimu kamili ya kujua kutofautisha makapi na bangi.

Kuna siku nimepita hapo kwa dogo asubuhi, niliucheki mzigo wake ni makapi yale yale tu ya jero, siwezi vuta uchafu huo, ni heri ninunue skank kitu orijino kwa elf 10 kuliko huu uchafu wa jero

Mvuta bangi mwenzangu upo?😂
 
Bangii ndio hzi au
JPEG_20220111_203952_6747030487059606336.jpg
 
Hapa jirani yupo muuza gongo bangi nk inapotokea mtu akienda kumsema polisi akichukuliwa asubuhi anahonga na hao hao wanamwambia aliyemtaja kuwa anauza haramu.

Hapo unakuwa visa hadi uliyeenda polisi unaikkmbia nyumba yako.

Amua mwenyewe la kufanya lakini ujue hao wavutaji watakufanyizia tu.
 
Mwite faragha umueleze kuwa aachane na hiyo kazi ya uuzaji wa bangi aendelee na hiyo nyingine sababu itamletea matatizo,na umwambie umesikia kuna mpango mkakati wa kumkamata ili aweke ndani ikibidi afungwe.

So kwa vile ww ni rafiki yake umeamua kumueleza ili achukue hatua mapema kabla hakijamsanukia.

Ukiona haelewei somo,tafuta askari polisi umueleze kama ulivyo eleza hapa kuwa hataki afungwe ila unataka kumtisha tu aachane na hiyo kazi so aende akiwa na Uniform then amwite faragha pia amueleze kuwa wamepokea malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya biashara yake hiyo haramu.

Hivyo anamuomba aachane nayo kabla hawajamchukulia hatua zinazostahiki.asipoelewa tena hapo mm pamoja na ww tunatakiwa kunawa mikono kama alivyofanya pilato.
Ukiona haelewei somo,tafuta askari polisi umueleze kama ulivyo eleza hapa kuwa hataki afungwe ila unataka kumtisha tu aachane na hiyo kazi so aende akiwa na Uniform then amwite faragha pia amueleze kuwa wamepokea malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya biashara yake hiyo haramu

Atakataa atakuambia mbele ya huyo Polisi wako kwamba yeye hauzi bangi na ili umkamate inabidi uwe na ushahidi ( bangi ) kumbuka pusha hakai karibu na bangi anayouza anaiweka mbali ili kukwepa kukamatwa na ushahidi ndo maana Kama alivyoeleza mwenye uzi hao watu wanajiamini Sana.
 
Hapa jirani yupo muuza gongo bangi nk inapotokea mtu akienda kumsema polisi akichukuliwa asubuhi anahonga na hao hao wanamwambia aliyemtaja kuwa anauza haramu.

Hapo unakuwa visa hadi uliyeenda polisi unaikkmbia nyumba yako.

Amua mwenyewe la kufanya lakini ujue hao wavutaji watakufanyizia tu.
Mamwera sehemu zote zinapouzwa bangi wanazijua sasa ukienda kushtaki utaulizwa anauza puli ngapi za bangi? Mwera akijua pusha anauza Sana bangi atakuja kuchukua mgao wake....!!!
 
View attachment 2077018

Mtaani kwangu kuna kijana yupo hapa kwa miezi miwili, yupo kwenye rika la miaka 24 hivi, ana frem anauza mahitaji ya nyumbani na vilevi, lakini biashara yake kuu yenye wateja wengi ni Bangi ambayo wanunuzi huvuta hapo hapo ama maeneo ya karibu, eneo sio la barabarani, huwa kuna watu wachche wanatumia hii njia.

Ni kijana mjanja mjanja, nilienda siku moja hapo kumcheki, kiukweli ana kipaji kikubwa sana cha kutengeneza urafiki, ndani ya dakika 4 tu tushazoeana na matani ya hapa na pale maana mimi pia nipo miaka 31 so ni kijana mwenzangu.

Sina tatizo na dogo ila ni hawa wavuta bangi, wengi hawana shughuli za kuwaingizia vipato, wakivuta bangi wanasizi tu, Pia bangi wanazovuta ni haya makapi ya shilingi 500 yanayouzwa karibu kila kona ya nchi, sasa hawa vijana kama hawajishughulishi na wanapenda bangi kinachofuata huwa ni wizi / utapeli, pia hatari kubwa ipo kwa ma house girl tunaowaachia nyumba zetu tukiondoka, wanaweza kurubuniwa na hawa vijana kirahisi.

Nyumba zipo 9 kwenye huu mtaa na zote zina fensi na mageti lakini kuna matukio kadhaa yamewahi kutokea watu kuibiwa nguo, tv, n.k. japo ni nadra, hatutaki yajirudie mara kwa mara.

Sasa ili kutatua matatizo hayo kabla hayajatokea mimi nimeona nishughulike haraka, ila kwa sharti moja tu, sitaki kushirikisha mkono wa sheria kwa sababu dogo anaweza kuishia mahabusu kesi yake ikasikilizwa 2040 na akienda mahakamani ni miaka 30 jela. Kinachonifanya nikwepe kutumia sheria ni hayo maisha ya Jela na Mahabusu kwa huku bongo, asikwambie mtu hizo sehemu hazifai hata kidogo, sikiaga tu flani yupo huko, sio kuzuri hata chembe.

Niliwahi kumwambia hio ishu itamuharibia life lakini dogo yeye anasema hakuna pusha asiejua hatari ya biashara anayofanya, anasema hajaingia kichwa kichwa anajua anachokifanya, kiufupi anajiamini sana lakini haiondoi uhalisia kwamba bado yupo hatarini.

Kijana ana miaka 24, haitakuwa vema mimi nihusike kwa yeye kutoka jela akiwa kamalizia ujana nyuma ya nondo.

Ni vipi nitaweza kutatua hili tatizo bila kushirikisa polisi.
Huyo pusha muache aendelee na kazi yake usimsumbue anajua anachokifanya.

Kuhusu wateja wake wapo aina tofauti Kuna vibaka hao hawakosi, lakini pia Kuna wateja wengine wenye shughuli zao za maana na heshima zao wanakuja kupata huduma hapo kwa pusha.

Nini cha kufanya
[emoji116]
Kwavile unalalamika kuhusu vibaka weka ulinzi nyumbani kwako alafu wekeni sungusungu (ulinzi shirikishi wa mtaani) hapo utakuwa umetatua tatizo.
 
Back
Top Bottom