Nawezaje kumtoa pusha wa mtaani bila kutumia Polisi, sitaki dhambi ya kumfanya mtu atoke jela akiwa mzee

Weka fence ya umeme kwako, hao mapusha hawatasogelea kwako.

Kifupi ni kwamba wewe imarisha ulinzi wa nyumbani kwako tuu basiii, mengine achana nayo.
Hatari i kubwa sana, hata watu wanaopita kwa miguu hapa wataanza kukabwa, pia hata ma house girl wanweza kurubuniwa na hawa watu wakatuvamia usiku maana wengi hawana shughuli za vipato na wanapenda bangi sana, mvuta bangi akiwa na kiu (arosto) ni hatari sana
 
Muelekeze tu kuwa biashara yake inaharibu vijana akili na kupelekea wao kufanya uhalifu hivyo yeye kama ataweza aachane nayo kama hawezi kuiacha basi wakae washauriane na wateja wake juu ya kuacha vitendo vya uhalifu mtaani na kama itatokea uhalifu wowote na ulishawaonya basi hatua kali zitachukuliwa, In piece tu ili baadae usije niweka kwenye history of your life kuwa ni part ya kuyaharibu.
 
Mvuta bangi mwenzangu upo?😂
 
Hapa jirani yupo muuza gongo bangi nk inapotokea mtu akienda kumsema polisi akichukuliwa asubuhi anahonga na hao hao wanamwambia aliyemtaja kuwa anauza haramu.

Hapo unakuwa visa hadi uliyeenda polisi unaikkmbia nyumba yako.

Amua mwenyewe la kufanya lakini ujue hao wavutaji watakufanyizia tu.
 
Ukiona haelewei somo,tafuta askari polisi umueleze kama ulivyo eleza hapa kuwa hataki afungwe ila unataka kumtisha tu aachane na hiyo kazi so aende akiwa na Uniform then amwite faragha pia amueleze kuwa wamepokea malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya biashara yake hiyo haramu

Atakataa atakuambia mbele ya huyo Polisi wako kwamba yeye hauzi bangi na ili umkamate inabidi uwe na ushahidi ( bangi ) kumbuka pusha hakai karibu na bangi anayouza anaiweka mbali ili kukwepa kukamatwa na ushahidi ndo maana Kama alivyoeleza mwenye uzi hao watu wanajiamini Sana.
 
Mamwera sehemu zote zinapouzwa bangi wanazijua sasa ukienda kushtaki utaulizwa anauza puli ngapi za bangi? Mwera akijua pusha anauza Sana bangi atakuja kuchukua mgao wake....!!!
 
Huyo pusha muache aendelee na kazi yake usimsumbue anajua anachokifanya.

Kuhusu wateja wake wapo aina tofauti Kuna vibaka hao hawakosi, lakini pia Kuna wateja wengine wenye shughuli zao za maana na heshima zao wanakuja kupata huduma hapo kwa pusha.

Nini cha kufanya
[emoji116]
Kwavile unalalamika kuhusu vibaka weka ulinzi nyumbani kwako alafu wekeni sungusungu (ulinzi shirikishi wa mtaani) hapo utakuwa umetatua tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…