Nawezaje kupata Leseni ya Biashara ya online?

Na je kuna gharama yoyote TRA kwenye kupata documents zote?
Ni lazima uende kwanza TRA watakuuliza baadhi ya maswali kulingana na aina ya biashara unayotaka kufanya....halafu watakupa maelekezo ya namna ya kufanya ...ni vigumu kukujibu hapa moja kwa moja kwa maana hatujui aina ya biashara unayotaka kifanya.....
 
nimetuma nyaraka nina wiki na nusu, hamna majibu. wajinga sana hawa.
 
nimetuma nyaraka nina wiki na nusu, hamna majibu. wajinga sana hawa.
Wala usiwalaumu kwa maana siyo wewe peke yako uliyetuma Kuna watu wengi sana na inabidi hao maafisa wapitie kwa usahihi document zote kutegemeana na wingi wa watu walio apply hasa kwa Dar kwa maana watu ni wengi ....

na nikuulize swali...Unajua majibu yakitoka utayapata wapi??

Usije kukuta majibu yalishatoka kitambo na wewe hujui unasubiria tuu...[emoji23]
 
si unakuwa umefungua account, unayapata pale pale kwenye account.
 
si unakuwa umefungua account, unayapata pale pale kwenye account.
Ndyo hivyo wanaweka tiki ya kijani kwenye ile Application yako ya kuwa Approved. na kama ukiona wanachelewa sana jaribu kuwapigia wakuambie shida ni nini...kama ni Wingi wa watu walio apply au ni uzembe wao kutoku approve application kwa wakati...
 
Wajinga nyie
 
Kiongozi ukitumia mfumo wa TAUS PORTAL hamna umuhimu wa kutumia BRELA?
 
Kuna ofisi ya Halmashauri nilifika kuomba leseni wakasema kwasasa mteja aombe mwenyewe kwenye mfumo #tausi.tamisemi.co.tz nikamwambia kwangu itakuwa ngumu kama kuna uwezekano msaada kwenye tuta, afisa akasema nimpe 40k, nikamuuliza hapo ndio itakuwa tayari nitasubiri leseni pekee, akajibu hapana 40k ni gharama zake tu.

Tukaanza kupatana, mwisho akasema nikamtafutie 15k, nikajiuliza kwani yeye anafanya vipi aweze na mimi nishindwe, nikaenda steshenari wakasema gharama zote 10k, wao watanipa control no nikalipie.
 
Bdo ulikuwa muoga ..wengine tumenunua tu bundle halafu kila kitu mpaka kuscan documents tukafanya kwa Simu....

Unachohitaji ni utulivu.

Hata uki google " Namna ya Kusajili biashara Tausi Portal" utapata maelekezo yoote 'A to Z' tena kwa njia ya picha....

Mimi nilipoenda ofisi za manispaa nikakuta kuna Wazee, na Watu wazima sana wanasubiria msaada nikaona aibu mwenyewe kijana mzima napanga foleni??
 
Hiyo scanning kwa simu hadi nirudi skul, mara wanasema iwe kwenye pdf, au ndio maana simu zinacamera zaidi ya moja!!!?
 
Hiyo scanning kwa simu hadi nirudi skul, mara wanasema iwe kwenye pdf, au ndio maana simu zinacamera zaidi ya moja!!!?
Hapana mkuu....scanner ya simu ukishascan kabla ya kusave inakuletea Option "Save as PDF"

Inategemea na ni scanner gani unayoitumia..

Ila kama unaona kutumia ya simu ni usumbufu basi Nenda stationary na simu ascan alafu akiwekee kwenye simu...

Ila hakikisha hiyo pdf isizidi ukubwa wa MB 1.8 .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…