Nawezaje kupata walau GB 10 za internet kwa siku kwa bei nafuu?

Nawezaje kupata walau GB 10 za internet kwa siku kwa bei nafuu?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
N.B: NI KWAJILI YA MATUMIZI YA KUONGEZA ELIMU NA TAALUMA.

Si ajabu wengi wakiwemo hata viongozi wanadhani internet ni kwajili ya upuuzi tu maana wengi kwenye hutumia internet kufanya vitu visivyo na faida mfano kudiscuss umbea kwenye magrupu, kufanya umalaya, video za x, kuwa waraibu wa muvi, games, etc.

Kuna upande mwengine ambao ni muhimu sana ambao unahusisha kuongeza maarifa, taaluma, kipato, n.k.

Kuna mitandao kama udemy, cousera, skillshare, n.k hii inatoa kozi kwa mtindo mzuri sana, kuna kozi kama za kufanya masoko kwa njia za kisasa kwa kutumia internet ambazo hata vyuo vyetu havifundishi, kuns kozi za kutengeneza apps, kuna kozi za kuingiza vipato mitandaoni, kuna kozi za lugha, n.k, n.k, n.k. ndi youtube nayo iko poa ila mitandao niliyotaja hapo awali kozi zinatolewa kwa mtindo mzuri zaidi.

Ningekuwa Dar ningetumia cable za fiber za elf 70 kwa mwezi internet bia kikomo kwa spidi nzuri ila tatizo ni kwamba nipo Mbeya.

Je, tupunguze vipi gharama?
 
Bei nafuu kwako ni sh. ngapi??
Inategemeana na wazo litaloletwa, binafsi nina ndugu yupo dar yeye anawalipa zuku kama elf 70 kwa mwezi, internet anayopewa haina kikomo na anaweza kudownload gb 1 ndani ya dakika 15 tu, ubaya ni kwamba hizi huduma zipo Dar maeneo ya mjini mjini tu, nipo mkoani huku Mbeya
 
Pia PAYPAL itakuwa mkombozi kwa sisi tusio na ajira.
Paypal ni kama mpesa ya dunia ila inasikitisha sana kwamba hadi leo hii wazee wa BOT wamekalia maskio wamelala usingizi wa pono kwenye hili swala, yani tunachoweza ni kufanya malipo tu ila kupokea hatuwezi arghhh!!! hii ndio sababu watu wanavuka mpaka kwenda kenya kusajili line za safaricom zinazorusu paypal, shida yote hii kwajili ya wazee wa BOT waiokomaa na mambo ya kizamani zamani
 
Paypal ni mfumo wa kulipwa kutoka nje, ni kama mpesa ya dunia, inasikitisha sana kwamba hadi leo hii wazee wa BOT wamekalia maskio wamelala usingizi wa pono lwenye hili swala, yani tunachoweza ni kufanya malipo tu ila kupokea hatuwezi arghhh!!!
Kwa nini tusidishe kelele mpaka watusikie ndugu?maana paypal ni kitu muhimu sana.
 
Kwa nini tusidishe kelele mpaka watusikie ndugu?maana paypal ni kitu muhimu sana.
Kelele zimepigwa tangu kitambo, ndio shida ya taasisi zinazolipa mishahara mirefu na wanawekana kwa kujuana kwamba yule ni mtoto wa kigogo flani, yule ni ndugu wa flani, n.k hata mama Samia aliwachana wana spidi ndogo sana kwenye ile ishu ya bitcoins, aliwaambia wananchi wana spidi kuliko wao wanaosimamia mifumo ya fedha hapa nchini, ile taasisi inabidi ifumuliwe upya tu, nachoona ni kwamba viongozi wengi wa pale ni wazee ambao hawataki mambo mapya
 
Paypal ni kama mpesa ya dunia ila inasikitisha sana kwamba hadi leo hii wazee wa BOT wamekalia maskio wamelala usingizi wa pono kwenye hili swala, yani tunachoweza ni kufanya malipo tu ila kupokea hatuwezi arghhh!!! hii ndio sababu watu wanavuka mpaka kwenda kenya kusajili line za safaricom zinazorusu paypal, shida yote hii kwajili ya wazee wa BOT waiokomaa na mambo ya kizamani zamani
Inauma sana mkuu
 
Inategemeana na waO litaloletwa, binafsi nina ndugu yupo dar yeye anawalipa zuku kama elf 70 kwa mwezi, internet anayopewa haina kikomo na anaweza kudownload gb ndani ya dakika 15 tu, ubaya ni kwamba hizi huduma zipo Dar maeneo ya mjini mjini tu, nipo mkoani huku Mbeya
Hahahah Zuku ipo ushuani tu kwenye mwambao wa bahari!
 
kwahiyo kuangalia movies na games ni upuuzi??[emoji23]
Lugha uliyoanza nayo ni ishara ya kukosa busara
Uwe unasoma neno kwa neno mkuu, nimesema uraibu (addiction) kuna watu wamegeuza muvi na games kuwa zoezi la kila siku, Mtu huyu huyu unakuta hajawahi kujisomea hata kitabu chochote cha kumpa maarifa ukiachana na vile vya darasani. hebu tuanze na wewe umesoma kitabu kipi, cha nani na ulijifunza nini??
 
Wabongo kwa movie utawaweza
 
Mkuu usiwapangie watu maisha.Usidhani unavyotumia wewe internet ndiyo matumizi ya maana sana kuliko wanaocheza game, kuangalia movies etc.Dunia hii ni huru, kila mtu afanye yake (bila kuvunja sheria) cha msingi hakuna anayemuomba mwenzake pesa ya ugali.Tusidharauliane.
 
Zantel wanakifurushi cha mwezi GB 10 kwa Buku 10 tu
 
Back
Top Bottom