Habari
Wakuu naombeni njia nyepesi ya Kupunguza Umalaya , kuacha nitakuwa muongo ..
Maana ni kitu ambacho nimegundua kinanirudisha nyuma sana kwenye maswala ya maendeleo yangu binasfi..
Napoteza pesa, muda na hata sometimes nahisi Kuna roho chafu nazipata nikiwa na deal na mbususu tofauti tofauti.
Kiufupi Uzinzi ndio changamoto kubwa inayo nifanye nishindwe ku progress mbele .
Sina mke , ila na watoto, naishi mwenyewe tu .
Naombeni msaada
NB: Kuoa sio mpango wangu.
Haitakusaidia chochote kupunguza uzinzi. Wazinzi, hata wanaofanya uzinzi mara moja kila mwezi hawataurithi ufalme wa Mungu
Katika kitabu cha 1 Kor 6:9-10 SUV Biblia inasema:
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.
Ni kweli kwa nguvu zako huwezi kuacha uzinzi. Lakini kwa neema na nguvu za Yesu unaweza kuacha kabisa uzinzi na dhambi zote nyingine. Fuatisha sala hii ya toba kwa moyo wako wa dhati, utaona kiu ya uzinzi inakatika sasa hivi. Omba hivi:
"Ee Mungu mwenye rehema, ninakuja mbele zako nikiwa mnyenyekevu na mwenye majuto makubwa. Nakiri kuwa mimi ni mwenye dhambi na nimekosa mbele zako kwa mawazo yangu, maneno yangu, na matendo yangu.
Baba wa mbinguni, ninaomba msamaha kwa makosa yangu yote, yaliyo wazi na yale nisiyoyajua. Ninatubu kwa moyo wangu wote dhambi ya uzinzi na dhambi zote nyingine. Sitaki kuzitenda tena kuanzia leo. Naomba unisafishe kwa damu ya Yesu Kristo, Mwanao mpendwa, ili niwe safi mbele zako.
Ninaamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zangu na akafufuka kwa ushindi, ili mimi nipate uzima wa milele. Leo hii nampokea Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Ee Yesu ingia ndani ya moyo wangu, utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu na neema ya kushinda dhambi zote kuanzia leo.
Asante, Mungu Baba, kwa upendo wako na neema yako. Asante kwa kunisamehe na kunipokea tena kuwa mwana wako. Asante kwa kunisikia na kuniokoa.
Katika jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru, Amina."
Kama umefuatisha sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Dhambi ya uzinzi haitakutawala tena. Ili uendelee na wokovu, anza kuhudhuria katika kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha maisha ya utakatifu na kweli yote ya Neno la Mungu, upate mafundisho yatakayokusaidia kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Ubarikiwe sana.