GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,645
- 10,867
Kiwanja kipo mbali na mkoa ninaoishi kwa sasa. Nina mtu atakayenisaidia kupokea hela kwa ajili ya malipo, au ninaweza nikaweka kwenye akaunti ya muuzaji kama ataona sawa.
Changamoto yangu ni kuwa ninataka jina langu na sahihi yangu kama mnunuzi ionekane kwenye mkataba huo. Siyo kwamba siwaamini ndugu walio jirani na eneo kiwanja kilipo, ila ni tahadhari tu. Nimeshawaona ndugu wa damu wakigeukana bila aibu. Wao watashiriki kama mashahidi!
Nifanyeje?
1. Ikiwa jina langu litaonekana kwenye mkataba kama mnunuzi lakini mtu mwingine akasaini kwa niaba yangu, itakuwa na mkanganyiko kisheria?
2. Kuna mbinu nyingine ya ziada?