Nawezaje kuwa Kijana Mwenye Mvuto?

Nawezaje kuwa Kijana Mwenye Mvuto?

Sidi J

Member
Joined
Mar 13, 2017
Posts
45
Reaction score
49
Habari wadau,

Mimi ni kijana wa miaka 30. Nimezaliwa kijijini na kukulia huko. Mjini wa mara ya kwanza nilikuja kwaajili ya masomo.

Pamoja na kwamba kazi yangu inanilazimu kuvaa kistaarabu, bado nahisi sijafikia vile viwango ya kuwa "gentleman" na natamani sana kutupia pamba kama baadhi ya vijana huko mtaani.

Naombeni ushauri wenu wa vitu kama; aina za mavazi (suruali, shirt, viatu, Tshirt nk), marashi na deodorant...pamoja na pigo zingine zenye mwelekeo.

Na hapa mjini Dar ninapata wapi hivi vitu (najua maduka lakini nataka vitu classic, siyo hizi zangu za Karume).

Shukrani
 
Kabla ya kukushauri nguo tuanze na...

Rangi yako
Urefu wako
Uzito wako

Aina za nywele, nyingi , kipara au wastani?
Rangi-mweusi kabisa
Urefu -167 CM (5.6 Ft)
Uzito - 80Kg

Nywele ni nyingi za kawaida tu ila zinakua kwa kasi (nanyoa kila baada ya wiki mbili)

Ndevu ni zile za O (kuzunguka mdomo)

Hapo mkuu naamini umepata picha
 
Unataka kuwa na mvutooo?.... mwanaume?[emoji1745][emoji1745]

Aseee[emoji848][emoji848]

NB

Ila wanaume wa dar wanajua kuharibu wakaka wa mkoani mweeeh[emoji848][emoji848]
Usiogope bhana.....naamini sijasema nataka kuwa "mrembo" mvuto kwa mwanaume ni sawa na kusema "muonekano wa mtanashati"

Hata sijalenga kumuharibi yeyote kwakweli.
 
Back
Top Bottom