Nilitamani nikwambie kua unitafute private ili nikuelezee namna ya kuanza safari yako ya programming/coding/developing, ila kwa manufaa ya wengine pia ambao wanatamani kua programmers nimeona niweke hapa.
kwanza, unatakiwa uwe na nia ya dhati kujifunza programming, angalau kwa siku unaweza kutumia masaa 10, kujifunza na kupractice coding! kaa ukijua programming ni about practice sanasana vinginevyo utapoteza muda tu na utaiona inakuchelewesha maana inachukua muda sana na dedication mpaka kuja kuina matokeo yake, kwa wastani ya practice ya masaa 10 kwa siku ukiwa na good mentor mwaka mmoja unatosha kwako wewe kuanza career kama junior programmer, [ nasisitiza usiwe na tamaa ikulipe mapema utaichukia mapema sana]
pili, kua na vifaa vya kujifunzia mfano PC na ni vizuri kua na reliable internet, imagine niko kwenye course ya software engineering lakini kuna watu hawana PC so you can imagine jinsi ambavyo wanapata tabu!
tatu, hakuna lugha bora kuanzia au kumalizia, tafuta kitu kimoja kulingana na mahitaji yako, mfano kama unataka kuingia field ya machine learning unaweza kuanza na PYTHON, hiyo ndo best ila kama ni webdevelopment huko inakua tofauti kidogo,
NNe, utakachoanza nacho komaa nacho hichohicho, usiwe distracted na over information usipaparike kugusa hiki mara kile, yaani leo umeanza PYTHON next week umekimbilia JAVASCRIPT hujakaa vizuri upo HTML sijui mara C++, hautafika kabisa ukishika kimoja komaa nacho mpaka uwe expert kifupi una specialize kwenye kitu kimoja maana huwezi kujua kila kitu hata wale ma-GURU hawajui kila kitu ni wameshika kimoja ndo wakawa best nacho.
Tano; ukiwa unaingia katika programming nashauri iishi programming yaan ifanye iwe sehemu ya maisha yako, mcheza mpira, mpira ni sehemu ya maisha yake, mlevi ni pombe, programmer ni practice(coding) kufanya projects nyingi nyingi haijalishi unafeli mara ngapi maana huko ni sehemu maalumu ya kujifunza kwa kukosea, na programmers wengi si wachoyo wa maarifa kabisa ukitoa hawa ma-whacky wanaokutisha, ila huko nje utakutana na watu ambao wana inspire amateurs kama sisi wapo tayari kukusaidia at anytime as long as you are willing to learn!, tumia sanasana Twitter kuwafollow programmers, huko utapata mpaka hizi bootcamps ambazo ni very helpful in your programming journey na nyingi ni totally free, ushindwe wewe tu.
mengine wataongezea na wengine.
MWISHO na muhimu zaidi tembelea tovuti hii
ALX Africa - Power Your Future in Tech hua wanatoa course ya SOFTWARE ENGINEERING ni full sponsored course, hii itakua msingi mzuri kwako kwa asilimia 100, hua inatolewa katika duration ya mwaka mmoja na requirements zake ni dedication of 70 hours per week [hyo ni minimum ila binafsi naona 70 yanazidi] watanzania tuko wachache huko kwenye course za tech ila wakenya na wanigeria wamejaa sana, so personally napenda watanzania tuwe wengi huko.
NIMECHOKA KUTYPE.