Nawezaje kuwa Wakala wa benki. Mfano NMB na CRDB

Habari zenu wakuu,

katika pitapita zangu nimeona mabango ya wakala wa NMB najua humu kuna watu wengi wanaweza nijuza je, vitu gani vinatakiwa ili niwe wakala wa NMB? Je ni mtaji kiasi gani au vigezo vipi kuna maeneo mengi potential kuweka hii biashara.

Natanguliza shukrani
 
Mkuu ngoja nikupe udambwi dambwi, maana nipo jikoni. Kwanza unatakiwa uwe mwanachama wa max malipo, yaani uwe na mashine ya max malipo, pia uwe na mtaji usiopungua milioni tano, mzunguko wako kwa siku, yaani eneo lako lisipungue milion moja, baada ya hapo jina lako litapelekwa BOT kupata APROVED, ngoja kesho nikipata nafasi, nitakuletea na commision zake kwa kila transaction unayoifanya, kwakweli inalipa sana ukipata eneo, maana comision zake ni za ukweli.
 
Ulisema kesho na leo ni siku ya saba,au kesho ipi?
 
Mkuu ngoja nikupe udambwi dambwi, maana nipo jikoni. Kwanza unatakiwa uwe mwanachama wa max malipo, yaani uwe na mashine ya max malipo, pia uwe na mtaji usiopungua milioni tano, mzunguko wako kwa siku, yaani eneo lako lisipungue milion moja, baada ya hapo jina lako litapelekwa BOT kupata APROVED, ngoja kesho nikipata nafasi, nitakuletea na commision zake kwa kila transaction unayoifanya, kwakweli inalipa sana ukipata eneo, maana comision zake ni za ukweli.
commision zipo kama zile za makampuni ya simu kikubwa ni kwamba banki kuu inaweka nguvu kubwa kwe uwakala wa banki ili kuifikisha banki kwa wananchi..mnaweza nipim ili niweze wapa maelekezo stahiki
 
tukikupim utapata shida kila MTU kumjibu weka vitu vyote hapa tufaidike sote acha ubinafsi ni hayo tu.
 
Habari wanajamvi, kwa wanaofahamu, eti ni vigezo gani vinahitajika ila kuwa wakala wa benk hususani nilizozitaja hapo juu,

1) inatakiwa uwe na mtaji kiasi gani kwa benki ya crdb na nmb ili uwe wakala wao (ufanye baadhi ya malipo au deposit kwa niaba yao)?

2) Wanatoa commission kiasi gani?
 
Unatakiwa kuwa na leseni ya biashara miaka miwili, tin, utambulisho wako, utambulisho wa/wadhamin wawili, 200k kwa ajili ya mashine ya kutolea risit, mtaji ni wewe, uwe na sehem ya kufanyia biashara. Ukihitaji mpigie 0717667790 kwa dar anakufuata. Hiyo ni NMB
 
upo sawa...
 
naongezea hapo kwa mtumiaji wa NMB aliye tumia kwa muda usiopungua miezi 6 au mwaka...
 
Usiwe mwizi kigezo kikubwa
Usitoe siri za wateja wako
Account yako bank iwe na profit yakutosha

For more info tembelea bank watakupa A to Z
 
Back
Top Bottom