Nawezaje pata/calculate square meter kwa eneo lenye pembe 4 lenye urefu tofauti?

Mfano eno lina 15m, 18m, 21m na 10m tafadhali wataalamu nipeni squre meter..
Mmh, kwa kweli hesabu ni janga la Taifa. Ungelikuea umelichora hapo watu wangekusaidia kirahisi sana. Njia rahisi sana hilo umbo ligawe vipande vitatu, yaani upate umbo la msitatiri 1 na maumbo mawili ya pembetatu. Baada ya hapo unatafuta eneo kivyake vyake na unakuja kujumlisha hizo areas ulizopata, hii ni hesabu ya darasa la 5B ambalo tulisoma mimi na Mh. Musukuma! Njia nyingine ni ile ya kutumia formula ya trapezoid. Kama ungekuwa umelichora hapa ingekuwa rahisi kukuelezea watalaam wa hesabu wapo hapa! Ambayo kwa kurahisisha formula unasema A=1/2(a+b)× h. Kwa heri mwalimu!
 
Ingia play store na download distance ana area measurements app.
Weka on location,ikionyesha "ready" bonyeza kitufe cha play,anza kuzunguka eneo lako na uishie ulipoanzia.
Kwenye vipimo chagua meter na area
 

Attachments

  • Screenshot_20260306-222617.jpg
    44.5 KB · Views: 22
Toa japo angle moja.

Kwa mfano kama 90° kati ya upande wa 15m na ule wa 18m...

Utasaidiwa hata na AI
Mfano eno lina 15m, 18m, 21m na 10m tafadhali wataalamu nipeni squre meter..
 
Haiwezekani.

Isoperimetric Inequality Principle.

Vitu vyote vyenye mzingo sawa (perimeter), si lazma vilingane eneo.

Umetupa perimeter tu hapo, Haiwezekani kujua eneo.

Kwa saab inategemeana na vimeunganishwa vipi hivyo vipande vinne vya kingo.

Chagua umbo moja kwa kuunganisha hizo kingo kwanza, tujue eneo limekaaje. Mfano, tujue urefu wa diagnal moja ( ncha mpaka ncha zinazotazamana ). Halafu tutatumia Heron's Principle.
 
Bila kujua urefu wa diagonal huwezi ku calculate area. Kwa lugha ya hesabu problem is indeterminate. Iwapo unajua urefu wa moja ya diagonals( zipo mbili) ,eneo ligawanyika triangles mbili. Hapo una calculate ukubwa wa kila triangle na kumjulisha kupata ukubwa wa eneo zima.
 
Offcourse kama hujachora inakuwa ngumu. Lakini unaweza kukadiria kama ifuatavyo. Una reactangle (pembe nne) moja na triangle (pembe tatu) moja hii ninkwa kukadiria. Tafuta eneno la kila moja halafu jumlisha. Angalia picha niliyo ambatanisha.
 

Attachments

  • IMG_20260309_205056_329.jpg
    302.9 KB · Views: 20
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…