Nay wa Mitego awatusi bongo movie

Yanapelekana kama hayana akili, watu wazima hovyo. Badala ya kuboresha movie zao wanalazimisha watu kununua uchafu wao. Mbona kina diamond wanaeleweka tu na wanasonga mbele na miziki ya inauzwa na kupigwa kama kawaida? Wanashindwa kuboresha kazi zao wanatafuta umaarufu wa kijinga kwenye majukwaa ya siasa na magazeti ya udaku kisha wanategemea kazi zao zitapendwa. Kwa style hii kuliko kununua cd ya bongo movie ni heri hiyo hela kuigawa bure.

Kwanza wasanii wenyewe hawajiheshimu wanategemea kukuza kazi zao kwa skendo. Wanaiga mambo ya ulaya kisha mimi niangalie wakati kuna uwezekano wa kuangalia ulaya halisi. Wanatoa movie hazina uhalisia hawataki kuwekeza. Gharama za kutafuta umaarufu ni kubwa kuliko wanazofanya kwenye uwekezaji. Mtu movie ya masaa mawili anataka kutumia mil10 kuitoa na wakati mwanamuziki video ya dakika 4 anatumia 50 au 100 mil halafu wanategemea kupata soko kwa kuzuia masoko ya nje.

Yaani kwa akili zao wanadhani mtu uache kununua fast and furious pale kariakoo uangalia movie ya Ray au Vicent kigosi aliyesuka nywele na kuvaa hereni halafi ana act yupo ofisi kubwa ya serikali, hakuna uhalisia wowote. Yaaani hawa bongo movie ukiangalia movie zao unashindwa kuelewa ni movie au ni komedi. Nachowashauri watoe movie wasubiri kipindi cha kampeni kisha wakaoneshe huko kwenye kampeni. Walitugawa watanzania kipindi cha kampeni leo wanataka tununue movie zao kirahis.
 
Walizoe kuhongwa si wanaume au wanawake wote walikuwa omba omba Sasa mambo yamebuma wanatafuta wa kufa nae
 
Wapuuzi sana hao bongo mavi hawana vipya sasa wanalalamika nini saf sana dogo umewachana wanatamaa ya pesa kuigiza no zero
 
Bashite kawaingiza wenzake chaka.Sasa baada ya wahindi kuitwa Central sijui hao Bongo movie watauzia wapi huo utumbo wao
 
Movie unajua kabisa inaishaje ndo niangalie? Ha ha haaa.

Movie ya action mtu anapigwa risasi kichwani analia usiniueee...haaa risasi ya kichwa?

Movie full kuiga mauchawi ya Nigeria...upuuzi.

Eti niache kitu London has fallen au Prison break niangalie Jumba la dhahabu?

Niache kumuangalia Jack Bauer nimuangalie Ray aliyejikrimu kwa rangi za Gold Star?

Wakwendreee....wakizipiga marufuku tutaziingiza hata kwa vichochoro...
 
Nilikuwa najiuliza siku nyingi kwa nini Ney anajitambua kuliko wasanii wengi!!? Juz juz ndo nimepata jibu. Kumbe ni halfcast wa kinyaki na kichaga.
Bila shaka na ww in miongoni kati ya hayo makabila mawili
 
Wanakataza movie za nje zisioneshwe ndani, halafu wanataka zao za "jini kukodi bodaboda" tuzidownload torrent.. Acha nishushe 24 legacy imetoka episode Mpya...
 
Muvi inaanza kuandikwa leo jumamosi jumanne iko sokoni ishakamilika part one na two
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…