Nayaandika haya huku moyo wangu unavuja damu. Uchungu mwingi sana

Nayaandika haya huku moyo wangu unavuja damu. Uchungu mwingi sana

Mshana Jr Naomba usome Story ya huyu Mwenzetu ambaye ni Marehemu utupe somo kidogo kuhusu roho ya mauti.
 
Hearing loss mkuu, sisikii vizuri
Pole sana kumbe shida ya watu wengi hivi? Sikuwahi kujua wala kuwaza
Ila Mungu kawapa kipaji cha kuandika
Mfano tu mpauko yani ukisoma bandiko zake dahhh anajua kuandika vyema na kupangilia haswa
Mungu amlaze mahala pema
Mkuu pls kama unashida/tatizo share na wenzio usikae kimya sawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukifika mahali ukahitaji msaada,usifanye kama mpauko (nitafute) uje PM

Nitakusaidia ila usije ikatokea hata siku 1 ukajiona mpweke,sawa Iddy.
Asante kaka kwa moyo wako. Hatua ya kujitoa uhai ni kubwa sana sidhani kama nitafika huko. Nitakutafuta IshaAllah
 
Siamini hii story, hasa alivyoandika kuhusu reactions za lecturers kwa sabsbu yeye kuwa kiziwi, na inakuwaje anasikia watu wakimsema?
 
Hearing loss mkuu, sisikii vizuri
Umefanya jitihada zipi na sehemu gani umekwama?
Humu kuna madaktari na wasamalia wema pia. Watakupa msaada wa kitaalam na wengine watakuwezesha. Hata mimi nina wajibu wa kukusaidia, sina kikubwa lakini nitakacho jaaliwa, nitakupa.
 
Dah Roho yake ipumzike mahali pema peponi.
Amepitia mengi na inatia uchungu.
Kwa wana jf wengine tupunguze mzaha watu wakija na shida humu kwenye majukwaa.
Watu wana shida kiukweli na kama tukisikiliza labda tunaweza kuokoana bila kujua.
Afande tall ni member humu hujafanya poa hata kidogo.
You had a chance to save a life,lakini ukafanya nini mzee umeyumba sana!
Anyways depression is real!
To all my brothers and sisters going through difficulties,keep your heads up!
Sina vingi lakini ukijikuta huelewi ni inbox kama lipo ndani ya uwezo wangu nitakusaidia na kama halipo nitakupa hata ushauri.
Rest In Paradise Mpauko.
 
Heshima kwenu nyote

Nimepokea kwa masikitiko msiba wa member mwenzetu Mpauko ..kijana aliyekuwa na ulemavu wa viungo pia aliyepitia changamoto nyingi katika kuishi maisha yake..Bahati mbaya sikubahatika kuona Uzi wake mpaka mauti yalipomfika .sio kwamba ningeona Uzi wake mapema ningezuia kifo kisitokee la hasha Bali ningekuwa na ushauri chanya ambao moja kwa moja ungeweza kupunguza ugumu wa makali wa maisha aliyopitia.. kama ningeshindwa kutoa msaada wa kiumchumi..



Nisikae sana uko kwa sababu mambo yameshatokea na sio msingi wa hii mada kulaumu yaliyopita Bali ni kuweka taratibu na mipango itakayosaidia kupunguza kama sio kuzuia hali hii kutokea..

Hali hii !!ni hali gani ninayozungumzia ?nimeona vitu vya ajabu sana vile wengi wetu tulivyopoteza utu katika jamii yetu.inawezekana wengine walichukulia kama utani ,utapeli na usiriazi wa kweli wakasaidia vile wanavyoweza ..hongereni kwa kuwa kila mtu alifanya aonavyo ni sawa..

Bado tuna nafasi kama jf members ya kurekebisha makwazo yasitokee japo hayana budi kutokea ila ole wake yule asababishaye hayo makwazo.ishu ya kujinyonga/kujiua ni mtazamo wako unauchukuliaje katika hali unayopitia .hapa ndipo panahitaji ukaribu na mhanga namna ya kuruka hicho kikombe.jamani kama huna ushauri bora ukae kimya kuliko kukolezea petrol kwenye moto unaowaka

Napendelea tutoe mawazo,maoni na ushauri kama jamii moja toka ngazi ya uongozi mpaka members. Binafsi ushauri wangu kwa matatizo ya aina hii yawe yanakuwapin mojawapo la jukwaa au uzi kupandishwa mara kwa mara.Vile viongozi itakavyowapendeza katika hili..itasaidia Uzi kuonekana na members wengi pia msaada utapatikana wa kutosha

Huku jf watu wanafahamiana vizuri jamani tusidanganyane sisi ni watu tusiojulikana.mhanga wa tatizo atatoa taarifa zake baada ya hapo makachero wa kujitegemea wataingia kazini kisha kuleta mrejesho yasemwayo ni ya kweli au tunapigwa kamba..hapo ndipo tutakuwa na nguvu ya kukoment na kureply bila kukurupuka kama ilivyotokea awali..Ni vizuri tukawasamehe wale waliochangia kifo cha marehemu kwa namna moja au nyingine ..wao watakwenda kulipwa na karma

Nawasilisha hoja ..GT ipende JF changia mawazo chanya JF isonge mbele ..usikoment kwa mhemuko

Naenda salama Mpauko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Screenshot_20200229-121231.jpg
 
Back
Top Bottom