Heshima kwenu nyote
Nimepokea kwa masikitiko msiba wa member mwenzetu
Mpauko ..kijana aliyekuwa na ulemavu wa viungo pia aliyepitia changamoto nyingi katika kuishi maisha yake..Bahati mbaya sikubahatika kuona Uzi wake mpaka mauti yalipomfika .sio kwamba ningeona Uzi wake mapema ningezuia kifo kisitokee la hasha Bali ningekuwa na ushauri chanya ambao moja kwa moja ungeweza kupunguza ugumu wa makali wa maisha aliyopitia.. kama ningeshindwa kutoa msaada wa kiumchumi..
Nisikae sana uko kwa sababu mambo yameshatokea na sio msingi wa hii mada kulaumu yaliyopita Bali ni kuweka taratibu na mipango itakayosaidia kupunguza kama sio kuzuia hali hii kutokea..
Hali hii !!ni hali gani ninayozungumzia ?nimeona vitu vya ajabu sana vile wengi wetu tulivyopoteza utu katika jamii yetu.inawezekana wengine walichukulia kama utani ,utapeli na usiriazi wa kweli wakasaidia vile wanavyoweza ..hongereni kwa kuwa kila mtu alifanya aonavyo ni sawa..
Bado tuna nafasi kama jf members ya kurekebisha makwazo yasitokee japo hayana budi kutokea ila ole wake yule asababishaye hayo makwazo.ishu ya kujinyonga/kujiua ni mtazamo wako unauchukuliaje katika hali unayopitia .hapa ndipo panahitaji ukaribu na mhanga namna ya kuruka hicho kikombe.jamani kama huna ushauri bora ukae kimya kuliko kukolezea petrol kwenye moto unaowaka
Napendelea tutoe mawazo,maoni na ushauri kama jamii moja toka ngazi ya uongozi mpaka members. Binafsi ushauri wangu kwa matatizo ya aina hii yawe yanakuwapin mojawapo la jukwaa au uzi kupandishwa mara kwa mara.Vile viongozi itakavyowapendeza katika hili..itasaidia Uzi kuonekana na members wengi pia msaada utapatikana wa kutosha
Huku jf watu wanafahamiana vizuri jamani tusidanganyane sisi ni watu tusiojulikana.mhanga wa tatizo atatoa taarifa zake baada ya hapo makachero wa kujitegemea wataingia kazini kisha kuleta mrejesho yasemwayo ni ya kweli au tunapigwa kamba..hapo ndipo tutakuwa na nguvu ya kukoment na kureply bila kukurupuka kama ilivyotokea awali..Ni vizuri tukawasamehe wale waliochangia kifo cha marehemu kwa namna moja au nyingine ..wao watakwenda kulipwa na karma
Nawasilisha hoja ..GT ipende JF changia mawazo chanya JF isonge mbele ..usikoment kwa mhemuko
Naenda salama
Mpauko
Sent using
Jamii Forums mobile app