Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna umri ukifika utaanza kuzipenda ndevu,hadi saloon utakua unaenda kuzichonga style mbali mbali!!Mimi niko kama wewe ila mi nachukia kuota ndevu tu still ni kijana mdogo tu.... I wish nipate dawa ya kuzifanya zisiote arghhh 😡
Usiogope sana Shikamoo! Siku hizi unaamkiwa na bado vyombo unapewa vile vile,huku ukiitwa Dadiiii wangu!!![emoji1][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mkuu unapitia situation kama Yangu, Kuna watu wakiniamkia nanuna kabisa, naona kuwa sistahili shikamoo zao. Kweli ujana maji ya moto, Shikamoo uzee.
Hapa UK wanachoma sindano inayoitwa botox inachelewesha kidogo uzee lakini furahi tu maintain mwili wako penda kutembea kwa miguu avoid kudrive jaribu kuondoa mawazo yasiyo na maana yoyote maana ukijipa mawazo unaziongeza mviNdugu zangu,
Nafikiri nipo katika wakati mgumu sana,nazeeka na nimeingiwa na hofu, nimegundua nauingia utu uzima, nimechukia, naogopa nahisi maisha ndio basi, kila nikipita nasalimiwa shikamoo, sipendi jamani wengine wananisalimia nawaona kama tunalingana,naogopa sana uzee.
Mvi zinabisha hodi kila kukicha, nimeanza kubadili mavazi niliyoyapenda sasa navaa kama mchungaji, sitaki lakini hakuna jinsi, mlioushinda uzee nitieni nguvu nahisi sipendwi tena nikipita hakuna anayenitazama kama zamani, naogopa kutongoza huenda nikatukanwa hadharani.
Mmh, mlioushinda uzee nisaidieni