Nazi nzima ni Agharabu ya Mbovu. Waliocheza Fainali ya Afrika wanachekwa na waliokosa kila Medali kwa Misimu 2 mfululizo

Nazi nzima ni Agharabu ya Mbovu. Waliocheza Fainali ya Afrika wanachekwa na waliokosa kila Medali kwa Misimu 2 mfululizo

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Ni ajabu na kweli ya kwamba kuna mashabiki, viongozi na wanachama wa klabu moja hapa nchini wamefanya sherehe ya kufurahia baada ya Yanga kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USMA Alger ya Algeria.

Watu hao ambao chuki na wivu wa maendeleo kwa Yanga vimewafanya watafute sababu yoyote ile ya kujifariji wamejikuta wakisahau timu yao kwa misimu 2 mfululizo wakikosa;

Medali yoyote ile ambayo ni rasmi.

Kombe lolote lile hata la kunywea kahawa.

Wenzao wamekusanya point 20 kwenye Club Ranking ndani ya msimu 1 wao wamesota misimu 4 na alama zao 35.

Wenzao wamecheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika wao wameshinda kombe la robo fainali kwa misimu 4 mfululizo.

Wenzao watavaa medali ya michuano mikubwa barani Afrika lakini wao wakikuonyesha ata medali ya kuiba kwenye iyo michuano niite mbwa.

Wenzao wanapiga hatua moja mbele kuelekea mafanikio ya soka la kimataifa wao wamedumaa hawana tofauti na jiwe, jiwe halikui, halisogei, llilipokaa ni hapo hapo mpaka lihamishwe.

Wenzao wanatengeneza timu ya kiushindani na sio maneno matupu na propaganda wao wamekuwa watu wa propaganda za wakina Mangungu na Ahmed Aly wakiaminishwa uongo kuwa wanayo timu bora inayowaleta wakina Manzoki kusimamia uchaguzi wasiibiwe kura na sio kusajiliwa.

Wenzao wameweka alama kimataifa isiyofutika kirahisi na kuandika historia wao itawachukua miaka na miaka kufikia level waliyofikia Wananchi ya kucheza fainali ya Afrika.

Wenzao wanakwenda kufanya maboresho machache ya wachezaji 2 au 3 wa kimataifa ili kuendelea walipoishia msimu ujao wao ndio kwanza wanakwenda kuacha zaidi ya wachezaji 10 na kuanza na moja kujitafuta na hapo ndipo timu ya wananchi inakwenda kuusimika utawala wake kwa mara nyingine tena.

Wenzao wanavunja benki kufanya usajili wa kishindo kusajili wachezai aina ya wakina Ranga Chivaviro wanaocheza ligi ngumu ya South Afrika wao rada zao wamezielekeza kwenye ligi dhaifu ya Rwanda kuwasajili kina Sarpong waliochangamka.

Siku zote akili kubwa itaendelea kuitawala akili ndogo ukidumaa umedumaa tu hata ukipewa lishe ya ukubwani ni sawa na kupiga rangi upepo, TCHAO!
 
Back
Top Bottom