Mwenyewe0000
Member
- Oct 30, 2020
- 51
- 99
- Thread starter
- #41
week ya 3 ( Siku 21) bila kupiga Punyeto.leo Siku ya 7 nimetimiza Week bila Kupiga punyeto.
Asante Mungu kwa kuwa unaendelea kunisaidia na kuniimarisha zaidi. Ninaweza kwa kuwa waniwezesha. Ngoja niweke NENO kwa wingi moyoni mwangu kwa kuwa sitamani kurudi nyuma bali kusonga Mbele.
Nazidi kuona kuwa inawezekana kuacha kupiga punyeto, na katika Siku 7 naona kuimarika. Asante Mungu.
Inawezekana, Inawezekana
Ninaendelea Kumshukuru Mungu kwa kila siku anavyonipagnia, Mambo Makubwa niliyoyafanya.
*Jumapili nilienda Kanisani nikatoa Sadaka ya Shukrani, pia Nikamuomba Mungu azidi kunisaidia kwa kuwa pekee yangu siwezi.
*Kuna wakati nilipitiwa kwenye jaribu LA kutazama vitu vinavyopelekea kujichua kwa tamaa ila katika kutazama ndani nikakumbuka kuwa nilishasema No kwa Punyeto nikaacha na kuendeleza kazi za kuwa busy
*Nimejifunza kupuuzia wanaosema huwezi kuacha, hiyo huwa hawaachi, na wenye kukatisha tamaa.
*Nimeamua kujifunza na kusikiliza kwa walioacha, na wanaotamani kuacha na wenye maneno ya kutia nguvu.
Ni maamuzi mazuri kuamua kuacha, Siku ya 21 Leo, Asante Mungu. Ukitaka kuacha kitu kibaya epuka kuwasikiliza wanao ona kuwa haiwezekani, jifunze kwa wanaoweza kukujenga kukushauri na kukutia moyo