Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,416
- 12,618
Mimi nimeanza kufuatilia huu mchezo mwaka huu(kuna jamaa yangu alinishawishi kuangalia),ilikua ni kwenye hatua ya PLAYOFF games...
GSW alikua anacheza na OKC...
Kwakuwa hiyo ndio ilikua game yangu ya kwanza kuiangalia nikajikuta niko upande wa GSW...
Baada ya hapo nikaja kuangalia game zote za fainali,kati ya GSW na Cavs...
Baada ya hizo games kuisha na Cavs kuwa washindi,nikatangaza humu kwamba nitakuwa shabiki wa GSW...
Nikapokelewa kwa mikono miwili na Tyta na Steph Curry ...
Mchezaji nayempenda zaidi kwasasa ni Steph Curry...
Kwakuwa ni mchezaji wa timu ninayoishabikia..!
Kwakipindi hiki kifupi nilichoanza kuangalia bball nimegundua wachezaji wanaopendwa zaidi NBA kwasasa ni Lebron James,Westbrook na Kyrie Irving..!
Timu inayopendwa zaidi ni Cavs..!
Asante kwa majibu yako mkuu.
Mfumo uko namna hii,
NBA ina timu 30, kila timu ina washabiki wake tufanye average ya mil 1 kwa kila timu (huu ni mfano tu),
Sasa kama timu ikiwa ni nzuri sana ina maana itakuwa inazifunga hizo timu zingine, wale washabiki mil 1 wa hiyo timu watakuwa wanafurahi sana, ila wale washabiki wengine mil 29 kwa vyovyote hawawezi kufurahi, isipokuwa kila hiyo timu nzuri itakapokuwa inacheza wataishangilia timu pinzani dhidi yake.
Msimu ulioisha GSW amezifunga timu zote kwenye regular season na kaweka rekodi ya kushinda gane 73 kati ya 82 huku Steph Curry akiwa ndo chachu ya hayo mafanikio, je unataka washabiki wa timu pinzani wafurahie?
Ni kama hata kwenye mpira, utakuta kwamba wachezaji wanaofanya vizuri ndo wanaoonekana kuchukiwa, au timu zenye kufanya vizuri zinakuwa zinaonekana kuchukiwa.
Kifupi ni kwamba, kama unanifunga, unanizidi uwezo kwa nini kwa nini nikushangilie?