NBA 2018/2019 is here...

Kama nilivyowahi kutoa ushauri, NBA inaelekea kule nilikotabiri...baada ya Christmasi ndio tutaweza kuona mwelekeo wa timu zinazotegemewa kufuzu kuingia ngwee ya pili, playoffs. Kwa kweli safari hii timu zote zimejipanga vilivyo tukiacha timu tatu nazo ni Chicago Bulls na Cleveland Cavaliers za Mashariki na Phoenix Suns kwa Magharibi.

Moto wa Toronto Raptors unaanza kupungua huko Mashariki wakati Boston Celtics ikizidi kuimarika huko. Kwa Magharibi kama kawaida michuano ni mikali kweli kweli ingawa mabingwa wa sasa Golden State Warriors wakianza kuonesha cheche zao. Tukae mkao wa kufaidi kwani hizi wiki mbili zijazo zitakuwa za kufa mtu.

Timu ambazo kufuzu playoffs safari hii ni za mashaka ni Cleveland Cavaliers ya Mashariki na San Antonio Spurs ya Magharibi. Timu hizi kama hazikuongeza nguvu si ajabu zikaishia njiani zisiingie playoffs safari hii. Hata hivyo hali hii itategemea zitakavyoweza kujiimarisha kwa kuwasajili wachezaji wapya wenye uwezo.
 
Wazee niaje? Kumepooza sana huku siku hizi!

Nani kaangalia game ya jana Rockets vs Warriors?

Hivi wale marefa ina maana hawakuona kabisa kuwa KD alitoka nje? Talk about kubebwa!

Final score inapaswa kuwa Rockets 135 na Warriors 132 [siyo 134].
 
Mimi navyoelewa GSW 134
Wazee niaje? Kumepooza sana huku siku hizi!

Nani kaangalia game ya jana Rockets vs Warriors?

Hivi wale marefa ina maana hawakuona kabisa kuwa KD alitoka nje? Talk about kubebwa!

Final score inapaswa kuwa Rockets 135 na Warriors 132 [siyo 134].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhaani hadi sasa timu zitakazofuzu kuingia kwenye playoffs zimeshaanza kujulikana ingawa kwa Western bado kwani kwa ugumu wa meshi si rahisi kutoa utabiri kama ilikvyokuwa miaka ya nyuma. Kwa Eastern naona Bucks na Raptors mambo yao tayari na ni vigumu wasisonge mbele labda kwa miujiza tu. Timu ya GSW itasonga mbele lakini safari hii si ajabu ikaupoteza ubingwa wa Western. Hata hivyo bado inayo nafasi ya kutetea taji lake na wiki ijayo tutaweza kuzitaja kwa uhakika zaidi timu zinazoweza kuingia fainali. Je watabiri mpo? Karibuni na ingieni kazini.
 
Kusema ukweli nimeshanhazwa na vipigo vya GSW aisee naona RAIA wametukamia sana na raia wetu wanaleta mazoea kwenye game za msingi

Sijui ndio wanasave energy for playoff au ndio nini.

Anyway bado naamini playoff watakuwa serious hasa kuliko sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona kocha wa Warriors anaipatapata kutoka kwa mashabiki wa the Dub Nation lakini sidhani kama kuna wasi wasi sana. Mpaka sasa watumbuaji wa GSW wamekuwa wakipeana zamu nani ashushe mvua siku hiyo lakini siku watakapoamua kutopokezana naona rekodi za ligi zitavunjwa na kupondwapondwa.

Juzi wamefanya kweli na kuwaacha wapenzi wakitabasamu baada ya kuwachapa Kings wa Sacramento nyumbani na hivyo kurudisha imani ya wapenzi hao. Siku hiyo mvua ya makombora ya masafa marefu ilivunja rekodi ya NBA baada ya vijana wa pande zote kurusha idadi kubwa ya makomora ya tatu tatu (3-pt) 41!
 
Daaah aiseee sijui ndo kikosi kimechoka au vipi mi naona

After this season baadhi ya players waachiwe waende zao hasa wale kuja wasio na mizizi katika timu

Wale damu changa zenye mwamko wa ushindani wakasaidiane na akina curry na klay na dreymond

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Vipi, umeuangalia mchezo wa leo kati seed one na seed two West? Kwa kweli Warriors nadhani wameamua kuwa sasa basi, hawataki tena utani. Trio ya Curry, Durant na Klay ni hatari sijawahi kuona, duh!

Mwisho wa mchezo Warriors 142, Nuggets 111. Qr ya kwanza vikapu 51 kwa 38!
 


Leo ilikuwa mwana ukome
 
Leo ilikuwa mwana ukome
Hebu fikiria siku ambayo Steph Curry, Klay Thompson na Kevin Durant watakaposema kama keba ni keba! Nawaambieni hapatakalika na historia ya basketball nchini Marekani (na duniani) itabidi iandikwe upya.

Hebu shuhudieni kidogo tu maajabu ya Steph Curry peke yake...


Na hivi ndivyo walivyoitafuna Denver Nuggets...

 

Hypothetical. BTW leo wako wanakula kichapo nyumbani kwao kutoka kwa NOP. Nadhani unaangalia game.
 
Hypothetical. BTW leo wako wanakula kichapo nyumbani kwao kutoka kwa NOP. Nadhani unaangalia game.
Eti unasemaje? Wanacheza na timu gani? Mchezo wa leo umeishaje? Bahati mbaya nimebanwa kidogo siwezi kuutazama kwa sasa, hebu tupe mrejesho.
 
100 Likes, mbona umepotea? Nina hamu sana ya kujua Warriors wamepigwa ngapi leo. Je mchezo bado unaendelea au umeisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…