NBA Playoffs

Status
Not open for further replies.

Utabiri umetimia.....woh hooo!!!!

Cavs - ok ngoja kwanza nikubali kuwa sijawahi kuangalia gemu yao mzima yoyote katika hizi playoffs mpaka jana. Hata hivyo bado nasita kusema chochote kuhusu uchezaji wao mpaka angalau nione gemu mbili zijazo. So far nasikiliza maoni ya wengine.

Magic - nashindwa kuelewa kwa nini hii timu watu wanaiona ni underdog of the three teams. Well, nathubutu kusema kuwa Magic wanacheza kitimu zaidi pengine kuliko timu zote 3. Wanaweza kuwa hawa-fancy moves zao, lakini wana gemu. Strategy yao inanikumbusha the Spurs (somehow).

I'm still standing by my yesterday's prediction - Nuggets win today!
 

So far quality ya opponents wa Cavs kwenye playoffs ilikuwa mbovu. Sasa unaona wakicheza na timu nzuri yenye uwiano? Matokeo yake ndo kama yalivyokuwa jana.

Magic sio underdogs kwa maoni yangu na bado nasema ni match up mbaya kwa Cavs. Magic wana watu wengi ambao ni wazuri kwenye 3pt shooting na hiyo imewasaidia sana kwenye playoffs hadi hivi sasa. Nadhani kwa hesabu za haraka haraka wana mtu kama nne hivi zenye uwezo mzuri wa kutungua hizo 3pts.

Nuggets hawashindi leo. Kobe is out to prove something.....
 
kid lebron bado saana kwanza mie siwezi kumlinganisha hata na kobe.....unajua kobe kama kwenye soka ni watu type ya akina zidane yaani timu inapozidiwa basi kila mchezaji anamuangalia yeye awaokoe......
....
ila orlando waliponea chupu chupu nao.....zile sekunde za mwisho mo william ule mtupo bado kidogo tu....
 

Ndio kufungwa huko mzee Yoyo, hakuna kuponea chupupchupu, ila mwisho wa siku LeBron atawasha moto na watapita.
Hao Orlando watatupa shida sie kwenye finals bora tuwapate CAVS maana match up na sisi hawatuwezi...
sisi= LA
 
atleast hii thread imerudi kwenye topic iihusianayo na kichwa chake maana nilichokaga hata kuifungua...kudos kwa hilo

tucheki cheki kusubiria tuone utaalam wa king kobe leo,but m sure game zikenda pepsi center ya tatu na ya nne denver hawatakubali kuzishidwa kirahisi
 
Mtaalamu naona machama yako ya nguvu tu,
Man U, LA . What about them Cowboys in football or NY Mets in baseball?
You seem to have a good test...
 
- Bado naamini Cavs watapita hapo kwa Magic, ila baso sijaelewa Kobe kama anaweza kuwapita Nuggets, lakini hizi gemu zinakumbusha sana enzi za quality basketball, yaani enzi za Dream Team ya M. Jordan.

Respect.

FMEs!
 
Ni kweli Mkuu FMES, enzi za Jordan Basket ilikuwa kali sana maana timu nyingi ziliipania sana Da Bulls kutokana na dedication ya Air Jordan na attitude ya ushindani mkubwa aliyokuwa nayo. Timu nyingi ziliona kuifunga Da Bulls ni kama fahari ya aina yake na MJ hakudharau mechi hata za timu ambazo hazikuwa na wachezaji Bora. Wakati wa Playoffs zile mechi ambazo zilikuwa too close to call katika sekunde za mwisho nilikuwa naikimbia TV ha ha ha ha maana nilikuwa na wasiwasi wa hali ya juu kwamba Da Bulls watashindwa ha ha ha siku hizi sina pressure kabisa naangalia tu naweza nikawa naifagilia timu moja au nyingine lakini siyo kama wakati wa Da Bulls.

Mchezo wa leo ni lazima Denver washinde kama wanataka kwenda kwenye 2009 NBA Finals vinginevyo watakuwa katika wakati mgumu mno. Bado naamini itakuwa ni Denver na Cleveland, lakini jana King James aliondoka uwanjani akiwa anachechemea haijukalini kama ataweza kucheza kesho na kama atacheza je atakuwa 100%? Pamoja na kupoteza mchezo wa jana bado naamini Cleveland watashinda, lakini wakifanya uzembe basi wanaweza oia kuondolewa. Sikuwaelewa kabisa kupoteza mchezo ambao walikuwa wanaongoza kwa 15 points halftime tena wakiwa nyumbani kwao. Ni masaa machache kabla ya game ya Lakers na Denver enjoy the game.
 

- Sawa sawa mkuu, tupo pamoja hapo!


William.
 
presha inapanda presha inashuka......
 
goo denver......sekunde 29 ni nyingi sana kwa kobe...
 
sassa hapa nitajua majuu wachawi...0.04 sec.....haya
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…