Natoa pongezi kwa Atlanta Hawks kwa kufuzu kuingia quarter fainali baada ya kuitoa Celtics ya Boston 4-2 na sasa mechi yake ya kwanza dhidi ya Cavaliers ya Cleveland siku ya Jumatatu, tarehe 2/5/2016, inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa Basketball.
Wakati huo huo leo timu sita zinaingia uwanjani tatu zikiwa kwenye hati hati ya kutolewa kama watafungwa. Timu hizo ni Clippers ya LA dhidi ya Trail Blazers ya Portland, Heat ya Miami dhidi ya Hornets ya Charlotte na Pacers ya Indiana dhidi ya Raptors ya Toronto.
Mpaka sasa timu zilizokwisha fuzu ni tano nazo ni Spurs, Cavaliers, OKC, Hawks na GSW. Timu ambazo tayari wapinzani wake wamejulikana ni hizo tatu za kwanza. GSW baada ya kuitoa Rockets ya Houston 4-1 inasubiri mshindi kati ya Clippers na Trail Blazers kumjua mpinzani wake..
Hakika leo asiye na mwana itabidi aeleke jiwe. Nazitakia timu zote husika kila la heri.