Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,416
- 12,618
Hapa umeongea Nzi, big up! Ninavyopenda vijembe, wee acha tu. Bila vijembe mbona jukwaa litapoa? Hapo juu tayari nimepewa kijembe...mbona sikusifia Paul Millsap alivyofunga points 45 na rebounds 13? Ni kweli sikufanya hivyo kwani mchezo sikuutazama (kumbuka narekodi zile ambazo nakosa kuzitazama), nitakapopata muda na kuuangalia sitasita kutoa pongezi.
Ushauri wangu kwa yeyote anayekwazwa akikutana na vijembe humu ni huu, kama moto wa jikoni huwezi kuuvumilia, mlango uko wazi, toka humo...ha ha haa! Bila vijembe jukwaa halinogi na toka leo naagiza ushabiki unaokosa vijembe ni marufuku katika jukwaa la burudani na michezo. Nitaendelea kutoa vijembe tena vizito kwa anayeponda timu yangu bila sababu za msingi, hapo sasa!
Ha ha ha, unajua kuna watu tumekua tunaangalia mipira kwenye vibanda umiza, culture ya ushabiki ni vijembe, kupondana nk. Na hata timu yako iwe nzuri vipi hukosi watu wa kuiponda na hiyo ni normal kwenye ushabiki wa michezo.
Sasa timu yako ikipondwa ukachukuliwa kama umedharauliwa ndo matatizo yanapoanza, unaanza chuki na kila anayeiponda timu yako.
Ushabiki ni vijembe.