Ni ushabiki tu Raimundo, sikujua watu wengine wanayachukulia tunayoandika so seriously! Wengine tunachangamsha tu jukwaa...with a light touch too, kama burudani. Mwambie na
Nzi asituchukulie namna hiyo...eti watu wanamwakia! Jamani ni ushabiki tu wa kiutani, hakuna sababu ya mtu yeyote kuzira. Naomba nichukue jukwaa hili kuomba radhi kama kwa michango yangu namkwaza mtu, hiyo si nia yangu.
Kwanza hiyo GSW au hata hao wachezaji wananihusu nini zaidi ya kuwa napenda mchezo wao? Kwani wakishinda au wakishindwa, maisha hayaendelei? Au wengine mmezama kiasi kwamba mkitaniwa kidogo tu mnaona mnawakiwa. Kwa upande wangu napenda tu kuchokoza mijadala na ni mwana michezo through and through...hatufahamiani tu lakini wengine tuliwahi kuwakilisha taifa katika michezo ya kimataifa.