NBAA: Ni kosa kufanya kazi za kihasibu na kikaguzi bila kusajiliwa na Bodi

NBAA: Ni kosa kufanya kazi za kihasibu na kikaguzi bila kusajiliwa na Bodi

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imesema kuwa hairuhusiwi mtu yeyote kufanya kazi za kihasibu na kikaguzi bila kusajiliwa na Bodi hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu jijini Dar es Salaam, Afisa Masoko na Mawasiliano wa Bodi hiyo, Magreth Kageya amesema ni kosa kwa baadhi ya Vikundi, Taasisi kuajiri watu na kuwapa vyeo vya Uhasibu na Ukaguzi.

Kageya amesema hairuhusiwi watu kupewa vyeo hivyo bila kupita ngazi maalum katika Bodi hiyo sambamba na kufikia ngazi ya CPA, ameshauri Taasisi, Mashirika hayo kuuliza kwa Bodi hiyo ni mtu wa aina gani anapaswa kuwa Mhasibu au Mkaguzi.

Kwa upande wake, Afisa Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka amesema Bodi hiyo kwa sasa ina Kitengo cha (Member Service) ambapo chini yake kuna Audit Quality Review (AQR) ambayo inahusika kukagua kuhakikisha Kaguzi zinafanyika kwa mujibu wa sheria za nchi na kukidhi viwango vya Kimataifa.

Hata hivyo, Bodi hiyo imeanzisha Mfumo wa usajili kwa Wanafunzi na Wanachama kwa njia ya mtandao, sambamba na usajili wa mitihani ya Bodi na kusajiliwa kwa Wanachama kupitia tovuti ya Bodi hiyo ambayo ni www.nbaa.go.tz
 
Nbaa wanataka ada za kila mwaka za vijana za bure bure.. huku wakiweka semina wanawalipisha tena..

Wahasibu kusajiliwa wote ngumu.. maana kampuni inakuwa na wahasibu mchanganyiko waliosajiliwa na wana cpa na ambao hawajasajiliwa wala hawana cpa.. kazi anaweza ifanya mhasibu asiesajuliwa ila mhasibu aliesajiliwa akaigonga muhuri

Hata kampuni kubwa za ukaguzi kama Kpmg, PWC, Delloite na Ernst and young zinaajiri sana wahasibu ambao hawajasajiliwa kabisa.. na wanawatumia sana kufanya kazi za kihasibu.. maana muhuri wa ofisi upo na waliosajiliwa wapo wataeekwa wao ndio waliofanya
 
1599119857550.png

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imesema kuwa hairuhusiwi mtu yeyote kufanya kazi za kihasibu na kikaguzi bila kusajiliwa na Bodi hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Maonesho ya 15 ya Vyuo Vikuu jijini Dar es Salaam, Afisa Masoko na Mawasiliano wa Bodi hiyo, Magreth Kageya amesema ni kosa kwa baadhi ya Vikundi, Taasisi kuajiri watu na kuwapa vyeo vya Uhasibu na Ukaguzi.

Kageya amesema hairuhusiwi watu kupewa vyeo hivyo bila kupita ngazi maalum katika Bodi hiyo sambamba na kufikia ngazi ya CPA, ameshauri Taasisi, Mashirika hayo kuuliza kwa Bodi hiyo ni mtu wa aina gani anapaswa kuwa Mhasibu au Mkaguzi.

Kwa upande wake, Afisa Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka amesema Bodi hiyo kwa sasa ina Kitengo cha (Member Service) ambapo chini yake kuna Audit Quality Review (AQR) ambayo inahusika kukagua kuhakikisha Kaguzi zinafanyika kwa mujibu wa sheria za nchi na kukidhi viwango vya Kimataifa.

Muungwana Blog
 
"ni kosa" na "ni marufuku" ni maneno yanayo tamalaki awamu hii ya kishamba.
 
Nba wanafanya kazi kama wanasiasa wakati ni chombo cha kitaaluma.
Kuna sheria inayotaka mtu ama taasisi yoyote inayopata mapato zaidi ya milioni 50 waajili mhasibu anayetambulika lakini hawafatilii ukiangalia wizi mwingi unaoripotiwa kuhusu wahasibu wengi sio wahasibu hali inayopelekea kuchafua taaluma ya uhasibu.
Sijawahi kusikia wakichambua ripoti ya cag wala kutoa maoni yao nini kifanyike kuzuiawizi unaoendelea kwenye taasisi za serikali.
Serikali ndio inaongoza kuajili watu wasio na sifa za kiuhasibu lakini wamekaa kimya bila kusema chochote.
 
Toothless institution. Hiyo walishalisema muda mrefu lakini hakuna ufuatiliaji wowote. Watu kibao wasio wahasibu wameajiriwa kama wahasibu.
 
Hahaha kazi zetu hazina job description hatuwi limited na professionalism. Naweza kuwa muhasibu leo, kesho nikawa ofisa mnunuzi, procurement officer.
Wasituharibie kazi.
 
Hawana lolote hawa. Shida ni hela kwa njia ya michango!
Na kweli kabisa. Huu ni mkwara mbuzi. Kuna wale wenzao wa bodi ya wagavi (PSPTB) nakumbuka mwaka jana walijifanya kuwafikisha mahakamani waliodaiwa kutosajiliwa au kuwa wakuu wa vitengo bila kuwa na sifa lakini hadi leo tunawaona maofisini wakiwa wanaendelea na kazi kama kawaida. Wakati wanawafikisha mahakamani walidai wana ushahidi 100%. Aidha ilikuwa kujionyesha kuwa wanachapa kazi, kutafuta hiyo michango ya kila mwaka au rushwa ilitembea. TAKUKURU na vyombo vingine wanapaswa kufanya uchunguzi juu ya jambo hilo huko PSPTB.
 
Kwenda kusajiliwa inakuwaje? Au ndiyo mnawapa mitihani konki

Ova
 
Back
Top Bottom