NBC Premier League' Namungo FC dhidi ya Azam FC, Ni vita ya kuwania nafasi ya tatu

NBC Premier League' Namungo FC dhidi ya Azam FC, Ni vita ya kuwania nafasi ya tatu

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania NBC Premier League, kupigwa leo March 16, 2022 kwenye Dimba la Ilulu mkoani Lindi, huku vita kubwa ikiwa ni kuwania nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

Namungo FC na Azam FC zote kwa pamoja zina alama 25 huku zikiwa zimecheza michezo 17 ambapo timu yoyote itakaposhinda mchezo wa leo itakaa kwenye nafasi ya tatu kwa tofauti ya alama na si tofauti ya mabao ya kufunga.

Namungo FC hawajapoteza mchezo wowote kati ya michezo mitano ya mwisho walizoshuka dimbani ambapo wameshinda michezo mitatu na kutoka sare michezo miwili.

Azam FC wanahitaji kupata matokeo ya alama tatu muhimu ili kurejesha timu kwenye morali ya ushindi ambayo imetoweka hivi karibuni, hivyo Azam FC wanahitaji kulifanya hilo kwa Namungo FC ambayo ipo kwenye fomu kwa sasa kuliko Azam FC.

Je? Ipi nafasi ya Namungo FC na Azam FC kwenye vita ya kuwania nafasi ya tatu NBC Premier League.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00 Jioni.
 
𝙰𝚣𝚊𝚖 𝚝𝚊𝚔𝚊𝚝𝚊𝚔𝚊 𝚝𝚞 𝚑𝚊𝚘 𝚠𝚊𝚙𝚒𝚐𝚠𝚎
 
Wote hao ndiyo washindani halisi wa Makolo kutafuta nafasi ya pili
We mchunga Ng'ombe wa Mayele unampinga Manara aliyesema ushindani mwaka huu ni Utopolo na Azam FC?
 
10' Namungo FC 1-0 Azam FC

Bao la Mohamed Issa Banka kunako dakika ya 02' ya mchezo.
 
23' Goooooooooooooaaal gooal

Azam FC wanasawazisha kupitia kwa Prince Dube, kazi bomba ya Kola

Namungo FC 1-1 Azam FC
 
Azam FC baada ya kusawazisha, wameamka sasa..! Pira Irizar
 
36' Goooooooooooooaaal gooal

Ismail Azaz Kader anaipatia Azam FC bao la pili, akiunganisha pasi nzuri kutoka kwa Zulu

Namungo FC 1-2 Azam FC
 
45+2' Kuelekea kuwa mapumziko kwenye Dimba la Ilulu mkoani Lindi

Naaam mpira ni mapumziko ambapo Azam FC wakiwa mbele kwa mabao mawili kwa moja.

Namungo FC 1-2 Azam FC
 
Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi ya hatari. Almanusura Azam FC waandike bao la tatu.

Charles Zulu amekuwa mwiba sana
 
Back
Top Bottom