Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Chama cha NCCR – Mageuzi kimemtangaza mwanachama wake Haji Ambar Khamis kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa huku Joseph Selasin akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa.
Mbali ya uchaguzi wa waili hao kushika hatamu za uongozi pia NCCR – Mageuzi imewatangaza wawili hao kuwa wagombea wenza wa Urais na Makamu wa Rais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Uteuzi wa wawili hao kukiwakilisha chama hicho kwenye uchaguzi huo ulifanyika ukumbi wa Mt. Gasper jijini Dodoma ambapo pia ndipo uchaguzi wa viongozi ulifanyika.
Wakizungumza baada ya kuchaguliwa kushika nyadhifa za juu katika chama hicho, Mwenyekiti ambaye pia ndiye mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama hicho Haji Ambar Khamis amesema “Tutafanya siasa za kistaarabu kwa kulinda na kuzingatia tunu za taifa ili kuwapa taswira ya aina ya uongozi ambao chama chetu unataka kuuweka madarakani pindi tutakaposhinda uchaguzi mkuu”
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Naye Makamu Mwenyekiti na mgombea mwenza, Joseph Selasin ameongeza kuwa “Amani, Upendo na Mshikamani ni Tunu za Taifa ambazo ni lazima tuzitunze na kuzienzi kwa nguvu zote ili Tanzania yetu ibaki milele, tukutane Oktoba kwenye Uchaguzi Mkuu”
Wagombea hao pia wameweka wazi dhamira yao ya kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba na kuahidi kushirikia na vyama vingine vya siasa nchini katika kuimarisha siasa nchini na kupinga vitendo vya mmonyoka wa maadili.