Nchemba amtakia maisha mema na afya njema Makamu wa Rais Dkt. Mpango baada ya kustaafu

Nchemba amtakia maisha mema na afya njema Makamu wa Rais Dkt. Mpango baada ya kustaafu

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Nadhani wangemuaga na Majaliwa tu naye akapumzike

===
Mheshimiwa Spika, nikiwa naelekea kuhitimisha hotuba yangu, napenda kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa weledi wake katika kuendelea kumsaidia na kumshauri Mheshimiwa Rais kuongoza Taifa letu.

Hakika mchango wake mkubwa katika ujenzi wa Taifa hautasahaulika.

Hivyo, tutaendelea kutumia busara, hekima, taaluma na uzoefu wake katika kuendeleza ustawi wa maendeleo ya Taifa letu. Nitumie fursa hii kumtakia maisha mema na afya njema baada ya kustaafu.

Naomba nimuage kwa neno kutoka katika Biblia Takatifu, Kitabu cha Hesabu 6:24-26 “BWANA akubariki na kukulinda; BWANA akuangazie nuru ya uso wake na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake na kukupa amani” Amina!
 
Ndio mlisema baada ya kustaafu kabla ya mwezi wa 8 ndio ataongoza nchi?
 
Back
Top Bottom