Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Sekta ya michezo ya Kamari barani Afrika inaendelea kukua kwa kasi, ikivutia wawekezaji, wasimamizi wa sheria na watafiti. Ukuaji huu unachangiwa na idadi kubwa ya vijana, upatikanaji wa intaneti na matumizi ya simu janja.
Ripoti ya GeoPoll ya Aprili 2025 inaonesha kuwa idadi kubwa ya watu katika nchi nyingi za Afrika wamewahi kushiriki betting angalau mara moja. Kwa mujibu wa takwimu za Worldometer za katikati ya mwaka 2025, ukubwa wa soko hili unaonekana wazi zaidi.
Nigeria inaongoza kwa idadi ya wanaobashiri, ikikadiriwa kuwa na zaidi ya watu milioni 168 wanaoshiriki michezo ya kamari (betting), ikichochewa zaidi na idadi kubwa ya watu. Kusini mwa Afrika, hasa Afrika Kusini, kuna ushiriki mkubwa kutokana na utamaduni wa kamari na mfumo madhubuti wa kisheria.
Nchi sita za Afrika zinakadiriwa kuwa na zaidi ya watumiaji milioni 440 wanaoshiriki michezo ya Kamari, jambo linalodhihirisha ukubwa wa sekta hii barani. Kwa Tanzania yenye Idadi ya Watu milioni 61.7 zaidi ya Nusu ya watu wake wanashiriki Kubashiri.