Nchi haipaswi kuendeshwa kisiasa. Afya ya mwananchi isifanyiwe kama mtaji wa kisiasa

Nchi haipaswi kuendeshwa kisiasa. Afya ya mwananchi isifanyiwe kama mtaji wa kisiasa

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau!

Nawasalimu kwa jina la Bwana na Allah.

Hivi mpaka lini serikali itaendelea kufanya siasa kwenye maswala ya msingi kama Afya?

Kila siku wanajinasibu kwamba matibabu ni bure kwa wajawazito na watoto, ila ukweli swala hili nilipingana sana na wife baada ya kuniaminisha kwamba watoto wanatibiwa bure maana hata wajawazito wanalipia mpaka kadi, kuna baadhi ya vidonge ambavyo inasemekana wajawazito wanatakiwa wapewe bure lakini hawapati bure, mpaka hizo neti za mbu ambazo zinatangazwa kwenye maredio hawapewi.

Binafsi nina watoto wawili mama tofauti mtoo wa wa kwanza sipo naye anaishi na mama yake kwa ss ana miaka minne tangu yupo mdogo nimekuwa nikituma pesa ya matibabu ikiwa anaumwa.

Ila sasa nilipopata mtoto mwengine kwa mama mwngine nikawa na mpango wa kuwakatia bima watoto ila huyu mke mdogo akanishauri nisifanye hivyo coz serikali inasema matibabu ni bure binafsi nikawaza labda inaweza ikawa kweli kudadeki jana katika harakati zangu nikapiga faida kama ya laki 2 ikabidi niende zangu kucheck mechi jioni narudi mtoto anaumwa ikabidi usiku nikimbizane zahanati ya jirani ya serikali yaani hauwezi amini ndugu laki 2 yote niliyopiga jana leo nimeamka na buku ten tu.

Naomba nieleweke kwamba sisemi kwamba nashinikiza watoto watibiwe bure hata kama serikali haina uwezo huo ila sio poa kuwatumia malaika kisiasa kwamba mnawatibu bure, malipo ni hapa hapa duniani.

Ndugu zangu niwaombe tuendelee tu kufyatua mitoto lakini tujue the healthy of your children rest on ya shoulder.
 
Kama wananchi watakuwa kimya CCM watatutesa mpaka mwisho wa dunia.
Kweli kabisa.
1608656075.jpg
 
Wewe vumilia tu maana ccm uliipenda mwenyewe.
Mlivyokuwa mnaimbishwa kuwa wataisoma namba mlikuwa mnaitikia tu kama mazuzu vile mlidhani wapinzani ndiyo wataisoma namba.
Halafu mwambie atutajie nchi ambayo haiendeshwi kisiasa na nini lengo la vyama vya siasa kama si kuongoza nchi!
 
Halafu mwambie atutajie nchi ambayo haiendeshwi kisiasa na nini lengo la vyama vya siasa kama si kuongoza nchi!
Kuongoza nchi kuelekea wapi? Kiongozi wa chama tawala kinachokusanya kodi, anaposema hatuleti maendeleo hapa sababu mmechagua chama pinzani anamaanisha nini? Nitajie nchi nyingine amabyo in siasa za hivi.
 
Mfano wako hapa unahusikaje na hoja mezani? Hoja yangu ni uongozi wowote wa nchi yoyote ni siasa hata kama nchi hiyo inaongozwa kijeshi au hata kidini.

Soma kichwa cha mada/habari utanielewa.
 
Mfano wako hapa unahusikaje na hoja mezani? Hoja yangu ni uongozi wowote wa nchi yoyote ni siasa hata kama nchi hiyo inaongozwa kijeshi au hata kidini.
Soma kichwa cha mada/habari utanielewa.
Hapa kwetu hakuna siasa nzuri ndio hoja ya mleta mada, wewe umengangania lazima kuwepo siasa.
 
Kujifungua watu tunajinunulia hadi gloves sembuse hiyo kutibu mtoto?
Gharama ya gloves ni ndogo Sana ukilinganisha na gharama halisi ya kujifungua. Gharama halisi ya kujifungua kawaida ni laki moja, wewe kuambiwa uchangie gloves za Elfu tano unaona ghali. Ninyi mnaogoma kuchangia gloves za Elfu tano mnaenda kulipia private hospital Zaid ya laki tatu kujifungua tuu.
 
Matibabu ya watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano ni bure kwenye vituo vyote vya kutolea huduma nchini. Acha kupotosha.
Hata mm ni kada ila kwenye ukweli najivua ukada ,afya sio swala la kisiasa ningeweza kupost mpk risiti za malipo hapa lakini sitofanya hivyo,najua ww hauna mtoto hata kama unaye you are irresponsible.
 
Wewe vumilia tu maana ccm uliipenda mwenyewe.

Mlivyokuwa mnaimbishwa kuwa wataisoma namba mlikuwa mnaitikia tu kama mazuzu vile mlidhani wapinzani ndiyo wataisoma namba.
Kuipenda tumeipenda wenyewe wacha ituue ,lakini mm kwenye , kusema uongo,siasa za kinafiki huwa siwezi.
 
Kujifungua watu tunajinunulia hadi gloves sembuse hiyo kutibu mtoto?
Gloves tu wakati wajawazito wanaenda mpaka na ndoo hospital ,yaani wamebakisha kuwaambia wajawazito waende na ufagio na maua kama primary vile😂😂😂😂
 
Kama wananchi watakuwa kimya CCM watatutesa mpaka mwisho wa dunia.

..tunatakiwa tupaze sauti ktk SANDUKU LA KURA.

..tunakosea sana kuwapigia CCM kura za Uraisi na Ubunge.

..tujiandikishe kupiga kura, na tujitokeze kupiga kura.
 
Back
Top Bottom