Nchi haipaswi kuendeshwa kisiasa. Afya ya mwananchi isifanyiwe kama mtaji wa kisiasa

Ni tiba gani hiyo aliyoipata hapo zahanati ambayo imeghalimu 190,000/=

Kwa level ya zahanati hasa ya serikali nakataa hilo otherwise watumishi wa hapo wawe wamekufanyia hujuma

Lakini pia uwe na habari kua vituo vya kutolea huduma asilimia kubwa ya fedha ya kuendeshea huduma inatokana na mapato/makusanyo ya kituo husika tena siku hizi mpaka mafunzo/seminar kituo ndio humlipa mtumishi wake akiitwa mafunzo/seminar

Kama operation ya mzazi C/S inafanywa bure ndio ije ishindikane hiyo homa kutibiwa bure?

Binafsi nina wasiwasi na watumishi wa hiyo zahanati
 
Mtoto ana malaria pia ana diarrhea ,vomiting,dehydration inabidi alazwe aongezewe maji pia apate dawa .
Labda kama una bima hauwezi elewa watu wasio na bima wapata shida gani pindi wanapoumwa.
 
Mtoto ana malaria pia ana diarrhea ,vomiting,dehydration inabidi alazwe aongezewe maji pia apate dawa .
Labda kama una bima hauwezi elewa watu wasio na bima wapata shida gani pindi wanapoumwa.
Kwanza malaria inatibiwa bure si kwa mtoto wala mtu mzima hilo uwe nalo kichwani kuanzia kipimo mpaka dawa na ni haki yako kuhoji pindi utakapotozwa gharama ya matibabu yoyote yanayohusiana na malaria

Pili hata kama ana dehydration ya aina gani sidhani kama mtoto anaweza akawekewa litre 5 za maji ambapo nusu litre ya hizo I/V fluids inauzwa sh 500 tu bei ya serikali lakini hata hivo kwa kundi la msamaha mfano mtoto huduma zote hizo ni bure

Kwahiyo hapo hata kama ungechajiwa pesa wala isingefika sh elfu kumi na hata kama ungeambiwa hizo dawa na vitu vyote ukanunue dukani wala isingefika elfu kumi na tano

Narudia tena ni hao watumishi wamekuhujumu
 

Na risiti nimepewa labda kama wasingenipa risiti kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…