Nchi hii Hakuna Daraja la Kwanza wala la pili. Wote Wana haki Sawa

Nchi hii Hakuna Daraja la Kwanza wala la pili. Wote Wana haki Sawa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!!

Moja ya mambo ambayo yananikera, yananifanya nisiishi Kwa Amani, nisiishi Kwa furaha ni kuona kundi Fulani linanyanyaswa. Kwa kweli katika vitu navichukia kuliko vyote ni kuona uonevu, unyanyasaji, ukandamizaji pamoja na dhulma ndani ya jamii.

Mimi hata awe mzazi wangu akileta mambo ya hovyo, akileta dhulma, ukandamizaji, unyanyasaji na mambo Kama hayo Kwa kweli namchukia, na wala sioni haya Kumkabili Kama Mungu aishivyo. Sipendi mtu asiyetenda Haki. Sipendi! Sipendi! Nachukia Sana.

Hata Kama sio Mimi nafanyiwa dhulma, unyanyasaji, uonevu lakini mwengine akifanyiwa huwa naumia mno.

Mtu hata alete maendeleo ya namna gani, hata ajenge pepo Duniani lakini Kama ni ya Dhulma hakika siwezi muona WA maana zaidi ya mtu wa hovyo tuu.

Watu wengi hudhani Mimi ni mpinzani hasa nilipokuwa kinyume na baadhi ya matendo ya awamu ya tano. Jambo ambalo sio kweli.
Mimi sio mpinzani, wala sio CCM na sitakuja niwe miongoni mwa Vyama hivyo.
Sipendi matendo yanayovunja haki za wengine.

Nchi hii Hakuna aliyezaidi ya mwingine, kila mmoja Kwa nafasi yake Kama Mungu aishivyo.
Aliyezaidi ni Mungu pekee.
Mambo yakufanya wengine daraja la pili sio mazuri.

Wengine wanafanya ni ruhusa, lakini wengine wakifanya ati ni kosa. Mambo hayaendi hivyo.

Hakuna la maana mtakalolipata dunia ingalipo Kama Mungu aishivyo.

Niliwahi kusema, kuna watu wanajiona wakubwa Kwa sababu ya kujidanganya kwao, huwezi ukawa mkubwa Kwa kuonea wengine, huwezi ukawa Mkubwa Kwa kunyanyasa wengine, huwezi ukawa Mkubwa Kwa kukandamiza haki za wengine,
Niliwahi sema, kacheo unakojidanganya nako hakatakusaidia chochote ukubali ukatae.
Mali ulizonazo hazitakusaidia lolote lile.

Haki na wema ndio utakaokusaidia.

Acheni kukandamiza wengine, acheni mara moja.

Tujaribu kuishi Kwa upendo, tupendane, mamlaka, Madaraka, vyeo visiwe chanzo cha kumuasi MUNGU.

Serikali yenye Nia ya kweli ya kuleta maendeleo kwenye jamii ni Ile inayofanya kila Aina ya njia kuwafanya watu wawe daraja moja. Iwe Kisiasa, kiuchumi, kijamii au kiutamaduni. Na huo ndio Uhuru.
Hatuwezi kuwa huru kwenye nchi yenye Madaraja.

Wito wangu hasa Kwa ninyi viongozi WA muda huu maana ni hakika hamtakuwa viongozi Daima; Acheni mambo ya kipuuzi, mcheni Mungu na kuzishika sheria zake. Msidhulumu, msikandamize wengine, wala msinyanyase Kwa maana Kama Mungu alivyomuaminifu, kipimo ulichokipima Kwa wengine ndicho utakachopimiwa na kufurika.
Tena utawa-cost mpaka na kizazi chako.

Watu tuache upumbavu

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro
 
Inauma sana. Hasa kwa watu walioshika madaraka toka 1961 mpaka sasa hawajiamini. Wanatawala ki mabavu kwa lugha za kizalendo.

Bahati mbaya WaTz nao wengi hawajielewie na ni waoga. Imekuwa mtaji kwao
 
Inauma sana . Hasa kwa watu walioshika madaraka toka 1961 mpaka sasa hawajiamini. Wanatawala ki mabavu kwa lugha za kizalendo.

Bahati mbaya WaTz nao wengi hawajielewie na ni waoga . Imekuwa mtaji kwao

Mtu akiwa muonevu, mdhulumati, mnyanyasaji huwaga simvumilii, namchukia na ananipa maisha magumu mno
 
Mtu akiwa muonevu, mdhulumati, mnyanyasaji huwaga simvumilii, namchukia na ananipa maisha magumu mno
Kuna mwingine alijiona mzalendo namba moja. Watu waliumizwa na kupotezwa chini yake. Lakini leo sote tuko mbele ya haki. Vya duniani vinabaki duniani hatuendi navyo kokote.

Leo hii kina Mbatia na wajumbe wake 30 wanazuiliwa kujadili Jambo lao. Huku Jana misikitini kumejaa. Leo wasabato na waprotestant wamejaza makanisa. Kesho ndiyo usiseme.
Kumbi za disco na michezo na hata mbio za mwenge. Mikusanyiko hiyo haionekani bali watu 30 wa nccr !!!.
 
Kuna mwingine alijiona mzalendo namba moja. Watu waliumizwa na kupotezwa chini yake. Lakini leo sote tuko mbele ya haki. Vya duniani vinabaki duniani hatuendi navyo kokote.

Leo hii kina Mbatia na wajumbe wake 30 wanazuiliwa kujadili Jambo lao. Huku Jana misikitini kumejaa. Leo wasabato na waprotestant wamejaza makanisa. Kesho ndiyo usiseme.
Kumbi za disco na michezo na hata mbio za mwenge. Mikusanyiko hiyo haionekani bali watu 30 wa nccr !!!.


Jambo la hakika Mungu hujibu Kwa uaminifu mkubwa, na Kwa wakati.
 
Back
Top Bottom