Nchi hii ilichezewa sana, au nchi hii itachezewa sana?

Nchi hii ilichezewa sana, au nchi hii itachezewa sana?

Maadam CCM bado wanaendelea kuiba kura kwa usaidizi wa state apparatus basi tutaendelea kuchezewa
Hivi huyu mama na yeye ataendeleza wizi wa kura?

Naona Mbowe tayari shamtolea kofia, au naye kaingizwa chooni?

Mimi nadhani Wapinzani wana nafasi sasa ya kukataa wizi wa kura zao, kama mabadiliko haya tunayoyaona yakianza yatakuwa ya manufaa kwa wote.
 
Nchi hii mwendazake akiiharibu acha tuifungue sasa....mataga mtulie kila zama kitabu chake
 
Hivi huyu mama na yeye ataendeleza wizi wa kura?

Naona Mbowe tayari shamtolea kofia, au naye kaingizwa chooni?

Mimi nadhani Wapinzani wana nafasi sasa ya kukataa wizi wa kura zao, kama mabadiliko haya tunayoyaona yakianza yatakuwa ya manufaa kwa wote.
Kwa mtazamo wangu, MAma hana cha kupoteza, yeye kuwa hapo alipo kwake ni pakubwa sana! Anaelekea kuwa flexible na analenga kujijenga kimataifa zaidi.

Naona pia CCM wengi hawamkubali sema tu ule unafiki wao ndio unawafanya waonekane wako pamoja ila wakipata nafasi "nzuri" wanaweza kumshangaza Mama.

Pia, CCM wako kwenye wakati mgumu maana ni kama vile nchi inatawaliwa na Wazanzibari, Mama akitawala Tanganyika na Mwinyi akiwatala Zanzibar. Kwa CCM wa kanda ya Ziwa inawaletea ukakasi sana.

Lakini poa nimewasikiliza Ccm kwenye Ufunguzi wa Kampeni Muhambwe, bado Point zao ni mbili, MOJA, Mwendazake alikua anaipenda Tanzania, PILI, Wapinzani wanachelewesha/wamechelewesha Maendeleo!

Kimsingi, naona CCM hawana jipya na hawana Umoja! Mama yuko tayari kujenga maisha yake ya uzeeni kuliko kuwafurahisha wapuuzi wachache.
 
Nchi tumepeleka kwa manyangau wanatuchora tu kule kwao.
 
Mpaka sasa,nchi iko mikono salama
JKM nakuomba Sanaa usikae mbali na Mama la sivyo......!
She can't manage herself.
 
Hayo maneno manee ya kwanza katika kichwa cha mada hii sio mageni kwetu, na wala sitopenda kuyaandikia kwa kirefu juu yake.

Haya manne niliyoongeza mimi, hata kama yanafanana na yale ya mwanzo, yanatofauti yake.

Kama ni kweli hii nchi "ilichezewa sana"; tulipoyasikia hayo maneno tulielewa nini?

Ni kweli hii nchi ilichezewa sana, na nani? Kuhusu nini? Nini kilifanyika tuache kuchezewa?

Hiyo ilikuwa ni wakati huo.

Sasa tena tunauliza: Hii nchi itachezewa sana?

Kwa nini tukubali kuchezewa tena, wakati tulishasema, tuliwahi kuchezewa!

Kama hatukubali kuchezewa tena, tumejiandaa vipi ili tusichezewe tena?

Au hatuamini kuwa kama nchi tuliwahi kuchezewa; ilikuwa ni uongo tu wa mtu mmoja hata kama alikuwa ni kiongozi?

Tunayo hakika gani kwamba kiongozi wa sasa anajua anayofanya, na kwamba atahakikisha nchi hii haichezewi tena?

Na tukibaini kwamba tunachezewa tena, tunazo njia za kujinasua na kuchezewa huko?
Watanzania wachache wasiowavumilivu na maumivu ya kuponya madhara ya kucezewa ndio huamua kuendeleza jaramba hilo kwa manufaa yao binafsi.

Watu hawa wafuatao ndio miamba wa uthubutu ijapokuwa nyota zao zilishushwa na kuzimwa ghafla

1. Bibi Titi Mohamed-Dar Es Salaam
2. Oscar Kambona
3. Mwalimu Julius Nyerere-Butiama Mara
4. Abeid Amani Karume-Unguja Zanzibar
5. Rashid Mfaume Kawawa-Lindi
6. Edward Moringe Sokoine-Monduli Arusha
7. Christopher Mtikila-Njombe
8. Deo Filikunjombe-Njombe
9. Dr.John Pombe Magufuli-Chato Geita
10 Chacha Wangwe-Mara
11. Dr. Wilbroad Peter Slaa-Karatu Manyara
12. Maalim Seif Shariff Hamad-Pemba Zanzibar
13. Amina Chifupa-Kigoma
14. Lucy Selina Lameck Somi-Kilimanjaro
15. Patrick Kunambi-Morogoro
16. Paul Rupia-Tanga
17. Tuntemeke Sanga-Njombe
18. Samwel Sitta-Urambo Tabora
19. Adamu Sappi Mkwawa-Iringa
20 Chifu Nduna Songea Mbano Luwafu-Songea
21. Mtemi Isike Mwanakiyungi-Tabora
22. Mtemi Mirambo Mtyela Kasanda-Tabora
23.Paul Milyango Rupia
24.Japhet Kirilo & Sarakikya-Meru Arusha
25. Mangi mkuu Thomas Lenana Marealle-Rombo Kilimanjaro
26. Chifu Kingalu Mwanabanzi-Kinole Morogoro
27. Omukama-Rumanyika
 
Niseme tu wazi hapa: Hiyo 'list' ni ya ajabu kwelikweli!
 
Mpaka sasa,nchi iko mikono salama
JKM nakuomba Sanaa usikae mbali na Mama la sivyo......!
She can't manage herself.
Hayo maneno ya mstari wa kwanza aliyasema huyo unayemtegemea na kumwomba asikae mbali na Mama...!

Mstari wa mwisho, "She can't manage herself," haieleweki una maana gani!

Rais amtegemee mtu mwingine kutawala? Hata JKM atasita kujiingiza kwenye maamuzi ya kiongozi, hata kama wamo kwenye chama kimoja.

Hii ni ngoma ya mama, ataicheza mwenyewe atakavyoona inamfaa, na akifanya mazuri atasifiwa yeye, akiharibu, lawama zote ni kwake na wala hazitakwenda kwa huyo unayedhani atakuwa anam'manage'.
 
Ni wakati wa wanawake jamani ..sote tudemke!
 
Nchi tumepeleka kwa manyangau wanatuchora tu kule kwao.
Leo hii, May 06, tayari jamaa wa huko wanadai wasisumbuliwe wakati wanapoingia kuvua samaki ziwani (Victoria) upande wa Tanzania.
Jamaa wanapiga kelele, sasa ziara ilikuwa ya nini kama hawataruhusiwa kuvua samaki ziwani bila bughudha!

Huu ni mwanzo, ngoja tuone na mengi mengine.

"Nchi hii itachezewa sana" hadi mama achanganyikiwe.

Hofu yangu kuu ni moja.

Wakati mama anatangaza kufungua nchi (hivi ilifungwa?); haielekei kwamba anayo mikakati na mipango ya kuzuia madudu yatakayotokana na 'ufunguzi' huo. Hapa ndipo panapotia hofu kubwa.
 
Sina sababu ya kupinga unayosema mkuu, ina maana basi tujiandae tu kuchezewa.

Kukwambia ukweli, hata mimi sioni tumaini lolote juu ya kuzuia kuchezewa. Hakuna mwenye ubavu huo kwa hali iliyopo sasa.

Ninaweza pia kukushangaza wewe, na pengine wengi wa wanaJF hapa nikisema kuwa tofauti zozote zilizokuwepo kati ya CCM na CHADEMA hazitakuwepo tena; kama zitaendelea kuwepo hizo zitakuwa ni tofauti ya ulaji tu basi. Kila mtu atapambana apate mkate wenye siagi.

Tatizo la Watanzania wengine ni watu wa kufikiria mabaya tu! Mama kaingia juzi tayari watu wanafikiria tutachezewa! kwa fikra za kizushi na bila ushahidi wowote!. Tunatakiwa tufikirie mazuri na jinsi gani ya kuleta maendeleo kwenye nchi zetu na tukianza kufikiria mabaya ndiyo yanatokea. Mambo mengi ni sisi wenyewe tunajiombea. Wananchi tujitume badala ya majungu na fikra za kimasikini na kujitafutia wachawi wenyewe. Tuache tabia za kulaumu laumu
 
Wakati tungali tunayawaza haya mapya anayoyafanya mama, inabidi pia tuwe tunarejea nyuma kutazama historia yetu kwa miaka kadhaa iliyopita.
Mimi nimeamua kutazama miaka aliyokuwepo mdarakani Kikwete na hali ya kule bungeni kwetu.

Kama sikosei, wakati huo wa miaka hiyo, ndio wakati tulipoanza kuwapata wabunge wengi waliokuwa wafanya biashara wakubwa hapa nchini.

Hivi kule Bungeni walikuwa wakitafuta nini?

Haraka haraka nakumbuka walivyokuwa wakihangaika na swala la uagizaji wa sukari..., kila ilipofika msimu wa uhaba wa sukari tuliziona juhudi zao zilivyokuwa zikienda.

Kuna mifano mingi mingine ya namna hiyo.
 
Tatizo la Watanzania wengine ni watu wa kufikiria mabaya tu! Mama kaingia juzi tayari watu wanafikiria tutachezewa! kwa fikra za kizushi na bila ushahidi wowote!. Tunatakiwa tufikirie mazuri na jinsi gani ya kuleta maendeleo kwenye nchi zetu na tukianza kufikiria mabaya ndiyo yanatokea. Mambo mengi ni sisi wenyewe tunajiombea. Wananchi tujitume badala ya majungu na fikra za kimasikini na kujitafutia wachawi wenyewe. Tuache tabia za kulaumu laumu
Tukashindane kwa kufanya "unyang'anyi", mbona hilo waTanzania hawakulizoea, ndio maana kuna hofu.
Tunatakiwa tufikiri mazuri: kuna uzuri katika wizi wa misaada kwa ajili ya COVID-19 kama ule uliotokea hapo KEMSA, na bado pasifanyike lolote?

Maendeleo hayawezi kuletwa na kazi za kuwadhulumu raia maskini.
Mimi nitakuwa wa kwanza kuunga mkono juhudi za mama kuhusu biashara halali kati ya mataifa, sio haya mawili tu, bali na taifa lolote endapo kama atakuwa na mipango madhubuti ya kuhakikisha kuwa nchi yetu HAICHEZEWI TENA.

Hapo juu unasema: "Mama kaingia juzi tayari watu wanafikiria tutachezewa!" Kuingia juzi, wewe huoni spidi ya mabadiliko yanayofanyika? Hata kama ni mazuri, kwa hiyo watu wasiseme kwa kuwa kaingia juzi?

Unakuwa na ujasiri wa kuandika eti "kwa fikra za kizushi na bila ushahidi wowote" Wewe unaishi nje, lakini hilo halizuii usijue kwamba anayofanya mama ni mapya na hakuna ushahidi wa yaliyotokea wakati palipokuwepo na maamuzi kama haya anayofanya sasa.

Kama wewe huyafahamu huna haki ya kuita usiyoyafahamu kuwa ni uzushi. Hopelee Kabisa.
 
Kuna watu mnajiona wenye maono kuliko. Lipi jema kwenu? Which initiative will be best for you?
The best initiative to me will be allowing business thrive while ensuring that benefits deriving from such activity permeate through to the common mwananchi, and not depriving him of the little that s/he has.

I am yet to hear any plans espoused by mama that ensures this will be the case as the new measures are being declared.
 
Leo hii, May 06, tayari jamaa wa huko wanadai wasisumbuliwe wakati wanapoingia kuvua samaki ziwani (Victoria) upande wa Tanzania.
Jamaa wanapiga kelele, sasa ziara ilikuwa ya nini kama hawataruhusiwa kuvua samaki ziwani bila bughudha!

Huu ni mwanzo, ngoja tuone na mengi mengine.

"Nchi hii itachezewa sana" hadi mama achanganyikiwe.

Hofu yangu kuu ni moja.

Wakati mama anatangaza kufungua nchi (hivi ilifungwa?); haielekei kwamba anayo mikakati na mipango ya kuzuia madudu yatakayotokana na 'ufunguzi' huo. Hapa ndipo panapotia hofu kubwa.

Kusema kweli kwenye hii kauli yake kwamba anakwenda kufungua nchi, ndipo hapo nilipoamini Mama hana alijualo pamoja na kuwa makamu kwa miaka yote sita!!
 
Kusema kweli kwenye hii kauli yake kwamba anakwenda kufungua nchi, ndipo hapo nilipoamini Mama hana alijualo pamoja na kuwa makamu kwa miaka yote sita!!
Sijui aliona nini huko kilichomnogesha akili kiasi cha kujisahau namna ile.

Anakwenda kuifungua nchi. Unaifungua kwa nani, 'cartels, tenderpreneurs'?

Kama yapo ya kurekebisha, rekebisha kwa utulivu, lakini sio kwenda na kujisahau kiasi kile ukiwa mkuu wa nchi.

Anatangaza, anakwenda kuifungua nchi, lakini hasemi ataweka 'safeguards' zipi ili nchi ifaidike na ufunguzi huo!

Mambo yafanywe tu kiholela, kwa kuwa nchi imefunguliwa?
 
Imechezewa, inachezewa na itaendelea kuchezewa unless...

"Avengers: EndGame"
Na ni katiba mpya itakayoondosha "umangimeza, uungu mtu na utwana" achilia mbali mageuzi ya kifikra.
Maana wako watu walifanya makosa yaliyodumaza Taifa lakini wanasifiwa kana kwamba walishuka toka mbinguni...
Makosa ya kikatiba yanatuponza sana hatujifunzi kwa Malaysia, Indonesia au hata Tailand nchi ambazo tulikuwa nao sambamba kiuchumi kabla ya miaka ya 80
 
Back
Top Bottom