Nchi hii ilichezewa sana, au nchi hii itachezewa sana?

Nchi hii ilichezewa sana, au nchi hii itachezewa sana?

Leo hii, May 06, tayari jamaa wa huko wanadai wasisumbuliwe wakati wanapoingia kuvua samaki ziwani (Victoria) upande wa Tanzania.
Jamaa wanapiga kelele, sasa ziara ilikuwa ya nini kama hawataruhusiwa kuvua samaki ziwani bila bughudha!

Huu ni mwanzo, ngoja tuone na mengi mengine.

"Nchi hii itachezewa sana" hadi mama achanganyikiwe.

Hofu yangu kuu ni moja.

Wakati mama anatangaza kufungua nchi (hivi ilifungwa?); haielekei kwamba anayo mikakati na mipango ya kuzuia madudu yatakayotokana na 'ufunguzi' huo. Hapa ndipo panapotia hofu kubwa.
Dah!

Mama inabidi acheze nao vizuri hawa jamaa si watu wazuri.
 
Mkuu nyuzi nyingi kwa sasa zinaponda kila linalofanywa. Ni vema tukaonesha namna bora zaidi ya kufanya jambo au nini kingepaswa kufanyika ili wenye nafasi wapate kujua.

Kebehi au kuponda haviepukiki ila mapokeo yetu yamekua hasi sana mpaka inatia shaka.

Namna ripoti ya CAG ilivyosomwa na kupokelewa na namna hatua za ripoti zilizochukuliwa, matumaini yote yamekufa.
 
Namna ripoti ya CAG ilivyosomwa na kupokelewa na namna hatua za ripoti zilizochukuliwa, matumaini yote yamekufa.
1. Wote waliokuwa wamemzunguka hayati walikuwa ni kinyume naye lakini hakuwepo mwenye ujasiri wa kumbishia chochote wakati akiwa hai ambao sasa ndio unawaona wakijifanya wanabadili mwelekeo wa fursa huru.

2. Machinga wanafukuzwa kama sio raia kwa sasa wakishiwa kwamba ni lazima walipe kodi kama wafanyabiashara wengine

3. Mama lishe wanatishwa kwamba lazima walipe sawa na wenye mgahawa unaolipia kodi

4. Madawa ya kulevya yamerudi kwa kasi ya mwanga huko jijini DAR hasa mitaa ya Masaki, Oysterbay, Msasani, Mikocheni, Mbezi Beach, Salsala, Goba, Mwananyamala, Kinondoni, Tegeta, Mbweni, Ubungo, Kawe nk tena mchana kweupe wazungu wa unga wanatamba nayo bila bughudha yoyote ile.

5. Watu wananyang'anywa ardhi halali waliyouziwa na wamiliki halali lakini anatokea tajiri mmoja sasa anakwambia hilo ni eneo langu na hati ni hii hapa-maajabu ya musa yanatendeka jangwani

6.Utatuzi wa migogoro, malalamiko sugu na uonevu hata yaliyo nje ya uwezo wa kisheria wanasukumiwa viongozi wasio na mamlaka

We need leaders who are ordinary citizens comforter, friend, motivating, confident nurturing, and protective to the marginalized rights. The polarity leaders shall not have our supoort at all
 
Dah!

Mama inabidi acheze nao vizuri hawa jamaa si watu wazuri.
Anao huo uwezo wa kucheza nao? Isijekuwa tumeweka matumaini makubwa kwa mtu ambaye uwezo wake ni wa kutiliwa shaka.
 
Anao huo uwezo wa kucheza nao? Isijekuwa tumeweka matumaini makubwa kwa mtu ambaye uwezo wake ni wa kutiliwa shaka.
Uwezo wake ni Mahusiano sio ubunifu wa vyanzo vya kukuza uchumi kwa faida ya nchi na watu wake ila kuneemesha na kuwafurahisha wageni na wafanyabiashara tu, basi
 
Hayo maneno manee ya kwanza katika kichwa cha mada hii sio mageni kwetu, na wala sitopenda kuyaandikia kwa kirefu juu yake.

Haya manne niliyoongeza mimi, hata kama yanafanana na yale ya mwanzo, yanatofauti yake.

Kama ni kweli hii nchi "ilichezewa sana"; tulipoyasikia hayo maneno tulielewa nini?

Ni kweli hii nchi ilichezewa sana, na nani? Kuhusu nini? Nini kilifanyika tuache kuchezewa?

Hiyo ilikuwa ni wakati huo.

Sasa tena tunauliza: Hii nchi itachezewa sana?

Kwa nini tukubali kuchezewa tena, wakati tulishasema, tuliwahi kuchezewa!

Kama hatukubali kuchezewa tena, tumejiandaa vipi ili tusichezewe tena?

Au hatuamini kuwa kama nchi tuliwahi kuchezewa; ilikuwa ni uongo tu wa mtu mmoja hata kama alikuwa ni kiongozi?

Tunayo hakika gani kwamba kiongozi wa sasa anajua anayofanya, na kwamba atahakikisha nchi hii haichezewi tena?

Na tukibaini kwamba tunachezewa tena, tunazo njia za kujinasua na kuchezewa huko?
Mzee niko pembeni yako hapa kwenye mkutano wetu wazee na Rais
 
"...mind shrunken..."? Do you even know what that is!
Dude, are you still challenging me to react to your senseless provocation? Impair and fix on your own, I am not a tutor to explicitly elaborate on what the figurative demarcation meant.
 
Kwani magufuli alikua anatoa hela zake mfukoni mwake? Mwacheni mama afanye kazi hizo imani mlizoamishwa na mwenda zake ndio zinawaletea mawenge
 
Dude, are you still challenging me to react to your senseless provocation? Impair and fix on your own, I am not a tutor to explicitly elaborate on what the figurative demarcation meant.
Eeenh Heee,
Wewe kweli ni kilaza, nilikuwa mwanzo natania, kumbe ni kweli wewe ni kilaza?
 
Back
Top Bottom