Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,459
- 100,799
Maadam CCM bado wanaendelea kuiba kura kwa usaidizi wa state apparatus basi tutaendelea kuchezewaNa tukibaini kwamba tunachezewa tena, tunazo njia za kujinasua na kuchezewa huko?
Hivi huyu mama na yeye ataendeleza wizi wa kura?Maadam CCM bado wanaendelea kuiba kura kwa usaidizi wa state apparatus basi tutaendelea kuchezewa
Kwa mtazamo wangu, MAma hana cha kupoteza, yeye kuwa hapo alipo kwake ni pakubwa sana! Anaelekea kuwa flexible na analenga kujijenga kimataifa zaidi.Hivi huyu mama na yeye ataendeleza wizi wa kura?
Naona Mbowe tayari shamtolea kofia, au naye kaingizwa chooni?
Mimi nadhani Wapinzani wana nafasi sasa ya kukataa wizi wa kura zao, kama mabadiliko haya tunayoyaona yakianza yatakuwa ya manufaa kwa wote.
Hakuna cha mshumaa hapa alieko apewe muda. Au arudi mtangulizi wake ama?Njia imefunikwa kwa giza baada ya mshumaa kuzimika ghafla
Watanzania wachache wasiowavumilivu na maumivu ya kuponya madhara ya kucezewa ndio huamua kuendeleza jaramba hilo kwa manufaa yao binafsi.Hayo maneno manee ya kwanza katika kichwa cha mada hii sio mageni kwetu, na wala sitopenda kuyaandikia kwa kirefu juu yake.
Haya manne niliyoongeza mimi, hata kama yanafanana na yale ya mwanzo, yanatofauti yake.
Kama ni kweli hii nchi "ilichezewa sana"; tulipoyasikia hayo maneno tulielewa nini?
Ni kweli hii nchi ilichezewa sana, na nani? Kuhusu nini? Nini kilifanyika tuache kuchezewa?
Hiyo ilikuwa ni wakati huo.
Sasa tena tunauliza: Hii nchi itachezewa sana?
Kwa nini tukubali kuchezewa tena, wakati tulishasema, tuliwahi kuchezewa!
Kama hatukubali kuchezewa tena, tumejiandaa vipi ili tusichezewe tena?
Au hatuamini kuwa kama nchi tuliwahi kuchezewa; ilikuwa ni uongo tu wa mtu mmoja hata kama alikuwa ni kiongozi?
Tunayo hakika gani kwamba kiongozi wa sasa anajua anayofanya, na kwamba atahakikisha nchi hii haichezewi tena?
Na tukibaini kwamba tunachezewa tena, tunazo njia za kujinasua na kuchezewa huko?
Kamfufueni mungu wenu wa chattoNjia imefunikwa kwa giza baada ya mshumaa kuzimika ghafla
Niseme tu wazi hapa: Hiyo 'list' ni ya ajabu kwelikweli!Watanzania wachache wasiowavumilivu na maumivu ya kuponya madhara ya kucezewa ndio huamua kuendeleza jaramba hilo kwa manufaa yao binafsi.
Watu hawa wafuatao ndio miamba wa uthubutu ijapokuwa nyota zao zilishushwa na kuzimwa ghafla
1. Bibi Titi Mohamed-Dar Es Salaam
2. Oscar Kambona
3. Mwalimu Julius Nyerere-Butiama Mara
4. Abeid Amani Karume-Unguja Zanzibar
5. Rashid Mfaume Kawawa-Lindi
6. Edward Moringe Sokoine-Monduli Arusha
7. Christopher Mtikila-Njombe
8. Deo Filikunjombe-Njombe
9. Dr.John Pombe Magufuli-Chato Geita
10 Chacha Wangwe-Mara
11. Dr. Wilbroad Peter Slaa-Karatu Manyara
12. Maalim Seif Shariff Hamad-Pemba Zanzibar
13. Amina Chifupa-Kigoma
14. Lucy Selina Lameck Somi-Kilimanjaro
15. Patrick Kunambi-Morogoro
16. Paul Rupia-Tanga
17. Tuntemeke Sanga-Njombe
18. Samwel Sitta-Urambo Tabora
19. Adamu Sappi Mkwawa-Iringa
20 Chifu Nduna Songea Mbano Luwafu-Songea
21. Mtemi Isike Mwanakiyungi-Tabora
22. Mtemi Mirambo Mtyela Kasanda-Tabora
23.Paul Milyango Rupia
24.Japhet Kirilo & Sarakikya-Meru Arusha
25. Mangi mkuu Thomas Lenana Marealle-Rombo Kilimanjaro
26. Chifu Kingalu Mwanabanzi-Kinole Morogoro
27. Omukama-Rumanyika
Hayo maneno ya mstari wa kwanza aliyasema huyo unayemtegemea na kumwomba asikae mbali na Mama...!Mpaka sasa,nchi iko mikono salama
JKM nakuomba Sanaa usikae mbali na Mama la sivyo......!
She can't manage herself.
Leo hii, May 06, tayari jamaa wa huko wanadai wasisumbuliwe wakati wanapoingia kuvua samaki ziwani (Victoria) upande wa Tanzania.Nchi tumepeleka kwa manyangau wanatuchora tu kule kwao.
Sina sababu ya kupinga unayosema mkuu, ina maana basi tujiandae tu kuchezewa.
Kukwambia ukweli, hata mimi sioni tumaini lolote juu ya kuzuia kuchezewa. Hakuna mwenye ubavu huo kwa hali iliyopo sasa.
Ninaweza pia kukushangaza wewe, na pengine wengi wa wanaJF hapa nikisema kuwa tofauti zozote zilizokuwepo kati ya CCM na CHADEMA hazitakuwepo tena; kama zitaendelea kuwepo hizo zitakuwa ni tofauti ya ulaji tu basi. Kila mtu atapambana apate mkate wenye siagi.
Tukashindane kwa kufanya "unyang'anyi", mbona hilo waTanzania hawakulizoea, ndio maana kuna hofu.Tatizo la Watanzania wengine ni watu wa kufikiria mabaya tu! Mama kaingia juzi tayari watu wanafikiria tutachezewa! kwa fikra za kizushi na bila ushahidi wowote!. Tunatakiwa tufikirie mazuri na jinsi gani ya kuleta maendeleo kwenye nchi zetu na tukianza kufikiria mabaya ndiyo yanatokea. Mambo mengi ni sisi wenyewe tunajiombea. Wananchi tujitume badala ya majungu na fikra za kimasikini na kujitafutia wachawi wenyewe. Tuache tabia za kulaumu laumu
The best initiative to me will be allowing business thrive while ensuring that benefits deriving from such activity permeate through to the common mwananchi, and not depriving him of the little that s/he has.Kuna watu mnajiona wenye maono kuliko. Lipi jema kwenu? Which initiative will be best for you?
Leo hii, May 06, tayari jamaa wa huko wanadai wasisumbuliwe wakati wanapoingia kuvua samaki ziwani (Victoria) upande wa Tanzania.
Jamaa wanapiga kelele, sasa ziara ilikuwa ya nini kama hawataruhusiwa kuvua samaki ziwani bila bughudha!
Huu ni mwanzo, ngoja tuone na mengi mengine.
"Nchi hii itachezewa sana" hadi mama achanganyikiwe.
Hofu yangu kuu ni moja.
Wakati mama anatangaza kufungua nchi (hivi ilifungwa?); haielekei kwamba anayo mikakati na mipango ya kuzuia madudu yatakayotokana na 'ufunguzi' huo. Hapa ndipo panapotia hofu kubwa.
Sijui aliona nini huko kilichomnogesha akili kiasi cha kujisahau namna ile.Kusema kweli kwenye hii kauli yake kwamba anakwenda kufungua nchi, ndipo hapo nilipoamini Mama hana alijualo pamoja na kuwa makamu kwa miaka yote sita!!
Na ni katiba mpya itakayoondosha "umangimeza, uungu mtu na utwana" achilia mbali mageuzi ya kifikra.Imechezewa, inachezewa na itaendelea kuchezewa unless...
"Avengers: EndGame"