Nchi hii tuna bora viongozi na si viongozi bora

Nchi hii tuna bora viongozi na si viongozi bora

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
3,474
Reaction score
3,744
Wasalaam,

Leo naandika kwa uchungu sana kuhusu tabia ya makampuni ya simu hasa hawa tigo kukwepa kodi kila baada ya miaka 5.

Serikali ina viongozi ambao wengi wapo pale kwa maslahi yao na si watanzania. Tangu jana nawapigia ndugu zangu waliopo tigo najibiwa kwamba namba unayopiga haipo, waziri yupo, TCRA wapo inakuaje watanzania waingie hasara kubwa kiasi hiki huku serikali ikiruhusu hawa wakwepa kodi kufunga line za watu .

Tukirudi nyuma kampuni hii inayojiita mixx leo ilianza kwanza kabisa ilisajiliwa kama MOBITEL, baada ya miaka mitano wakaruka kodi wakajiita BUZZ, baada ya miaka kadha wakaruka kodi wakajiita TIGO, leo hii wamerudia mchezo ule uke na kujiita Mixx.

Swali langu ni kwamba ina maana serikali haijui kweli kama kuna watanzania wamefutiwa namba zao na hawa mix? Yaani unaambiwa kabisa hii namba haipo. Ukirudi kwenye huduma za kipesa ni yale yale miamala inagoma na kutusababishia watanzania hasara kubwa sana huku viongozi wetu wakifaidi 10% kutoka mixx na kuziba masikio yao huku wakivaa miwani za mbao.
 
Katika vitu vinne alivyosema Mwl JK Nyerere vinahitajika ili Nchi iendelee, vilivyopo ni 1. Watu 2. Ardhi ambavyo havipo ni 1. Siasa safi na 2. Uongozi Bora.
 
Back
Top Bottom