Nchi hii watembea kwa miguu na abiria hatuna haki kabisa


Sijui ndio dua zao hizi
 
Uwepo ustaarabu huwezi kulazimisha kupendwa kwa kuruhusu watu kuvunja sheria na kufanya biashara maeneo hatarishi!? No sawa kuruhusu watoto kulala sebuleni na mambo yote sebuleni!! Hawa mameya kazi yao nini!?
 
Sisi machinga tuna kitambulisho chetu, tumeuziwa 20,000.

Nyie watembea kwa miguu mnakitambulisho gani maalum ?

Nasema hivi mtuguse tunuke🤣🤸🐒
 
Jiwe alivyokuwa waziri wa miundo mbinu alikataa kabisa njia/barabara za waenda kwa miguu zisijengwe eti ni anasa.
Kuna ubaya wa mtu nachuki juu ya mtu. Zaidi ya 30% ya barabara za rami nchini zimejengwa magufuri akiwa kwenye hicho cheo. Hivyo mbona mi siyaoni hayo mabarabara yasiyo na nafasi ya mtembea kwa miguu

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Dar kuna masoko ya kisasa kabisa yanajengwa lakini watu mabarabarani hawapungui, kuna soko kubwa kabisa pale karibu DIT, magomeni usalama napo pana soko la kisasa. Hao watu wapungue aisee.

Sasa imekua ni kawaida kufungua biashara kwenye njia ya waenda kwa miguu. Bodaboda zinapita huko baiskeli zinapita uko, kukiwa na foleni gari ndogo pia zinapita uko,gutaa yaani sasa inageuka kua kama uwanja wa vita myembea kwa miguu unakwepa mishald tu ukikaa vibaya boda anakuvaa au ukanyage bidhaa za watu bahati mbaya ulipishwe kwa makusudi.
 
Utashangaa wakuu wa mikoa wapo na serikali ipo ila kimyaaaa, wako bize kuibia nchi na wananchi wake.
 
Wanunuzi wengi ni wafanyakazi wa maofisini. Muda wa kwenda kule hawana. Hao jamaa inaonekana ni msaada kweli kwao. Nenda Mbagala mwisho uone.
 
ukiwafukuza wana msemo wao kuwa sisi ni wajane tunasomesha tumekopa tutaenda wapi
 
Baada ya kuwasomesha namba watu na kuuwa uchumi vijijini kwa kuharibu biashara ya mazao, kuharibu mijini kwa kutaka matajiri wawe masikini wengi walikosa kazi.Tumbo halina likizo ikalazimika waliokosa ajira wageukie umachinga Ili njia za chooni zisiote nyasi.Wanasiasa uchwara wasio weza siasa za hoja wanaona fursa ya kupata kura za watu waliowasababisha wakose ajira viwandani na mashambani.
Wakawaruhusu wafanye biashara popote kwa kuwapumbaza kwamba wanawasaidia nyuma ya pazia ikiwa ni kupata kura zao.
 
Wanunuzi wengi ni wafanyakazi wa maofisini. Muda wa kwenda kule hawana. Hao jamaa inaonekana ni msaada kweli kwao. Nenda Mbagala mwisho uone.
Kwahiyo nchi ni ya watu wa maofisini tu?? Tufate sheria sio mazoea mkuu.
 
Hao ni Wapiga Kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…