Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

Tatizo letu ujinga umekithiri... Uchawa umezidi... Woga umezidi! Imani potofu imekolea kwa ccm na viongozi wake!
Yaani katikati ya madhila yote uliyosema bado wananchi wengi wanaamini kuwa system iliyotufikisha hapo ndiyo itakayotutoa hapo!
Ingekuwa kwingineko wananchi wangeshajichukulia maamuzi mkononi!

My people; Tuamke tupambana na udhalimu tunapouona! Viongozi si malaika! Serikali au vyama si tawi la MUNGU useme kuwa ukiwapinga utakoswa kabisa pa kuishi milele!

Tuwapinge sasa kabla madhara hayajawa makubwa zaidi!
 
Mhhh...
Hivi ukinunua kwa rejareja na ukinunua in bulk...VAT inapungua?..

madawa yanatozwa kodi?

unataka kusema Serikali/mkusanya kodi haleti huduma kwa wananchi au?elimu bure ni nini ile?kwa mfano...mzazi kuchangia elimu ya mwanae tatizo ni nini?

Nnapoweza kukubaliana na wewe ni wakulima kupata ahueni fulani either kwenye mbegu ama mbolea ili kukuza kilimo/uzalishaji..na Serikali ina uwezo huo naamini,through subsidies

Ngoja wataalamu waje lakini...
 
Mkuu Kalamu1 leo nikupongeze kwa hoja. Ni kweli tatizo lipo Serikalini na tatizo hilo linajengwa pia na wabunge wetu ambao kwa kujua ama kutokujua hawalijengei hoja za kitaalamu kulitatua. Wabunge ndio hasa wakulaumiwa maana suala hili linawahusu Watanzania walio wengi ambao ni wapigaji kura wao, kwa watumishi wa Serikali wao huangalia masilahi yao kama mishahara minono, mikutano na warsha, mafao makubwa baada ya kustaafu kn. Ni wakati wa Wabunge kulitafutia ufumbuzi.
 
We kichwa ngumu, sasa hiyo bulk unahisi ukilipa usafir mil. 1.5 ukigawa kwa gunia unapata bei gani??
Au unalopoka tu.??
Tatizo inawezekana unabishana ila unakuta hujawahi kodisha hata Fuso wewe ukaweka mafuta na kumlipa dereva. Ujuaji mwingiii na kuilaumu serikali wakati wao wameshiba na mishahara minono. Amka, hii nchi ina mpaka usafiri wa bure as long as mzigo ulio nao una faida na unao mzigo wa kutosha.
 
Soma vizuri. Labda nikwambie tuu Mimi ni mfanyabiashara wa mahindi na hapo nimekupigia hesabu ya gunia moja kati ya mzigo mzima ambapo kwa Safari moja gari inabeba gunia 280-300
Naelewa yanayokukuta na pole na mapambano.....

Hizo gunia chache sana, lazima uumie na usafiri maana huwezi hata tangaza tenda na kampuni za logistic na ufinyu wako wa elimu na connection kujua wapi upeleke mahindi.

Unatakiwa kujua kuwa wakati nchi inasema usitoe mahindi nje kuna wenzako wanajua namna ya kuyauza.... wewe unawatajirisha wao kwa kuwapa kwa bei nzuriiii ya faida. Sasa utafute hiyo elimu na ongeza production.
 
Mkuu jua kuwa huyo wa bulk halipi VAT bali anakusanya VAT kwa niaba ya Serikali, mlipaji VAT ni mlaji wa mwisho. VAT ni kila kitu nini madawa. Mrejesho halingani na makusanyo, maana madawa ya hospitali, maji, umeme, ada na michango ya shule, nauli za usafiri, vivuko, mbolea na pembejeo zake, nk vyote vina muhusu. Kiongonzi kwa vyazo vya mapato tulivyonavyo LEO, maana Serikali inauwezo wa kutoa huduma hizo bure walao NUSU ya zile za Gadaf wa Libya. Lakini matumizi ya Serikali (Recurrent budget) ni kubwa.
 
Lawama zote kwa Awamu ya Tano iliyowafanya wawekezaji na Wafanyabiashara maadui. Leo Kenya wananjaa lakini walishaagiza Mahindi Brazil, wanalima Congo na Zambia unayo ya kutosha. Ya kwetu tutapeleka wapi na hatuna Mifugo ya kuyamaliza
Si mama yenu alienda mkasema karudisha mahusiano? Mpaka akili itawakaa nchi sio nyumbani kwako! Urafiki na kenya ni unafiki tu! Hakuna urafiki hapo ila watu mapimbi ndo huwa wanaaminishwa hivyo!
 
Si mama yenu alienda mkasema karudisha mahusiano? Mpaka akili itawakaa nchi sio nyumbani kwako! Urafiki na kenya ni unafiki tu! Hakuna urafiki hapo ila watu mapimbi ndo huwa wanaaminishwa hivyo!
Mkuu mbona unamlaumu jirani yako kwa vitu ambavyo havimuhusu? Kwani wewe ulikuwa unalima mahindi kwa ajili yake una oda yake ama ana hati miliki ya kununua mahindi yako? Unafiki wake upo wapi?
 
Mfumo kufeli ndo hii pole,nimekuwepo kigoma,rukwa sumbawanga kilio kikubwa hicho gunia 20000, niliumia sana na kunawahuni inside government wanafaidika na huo mchezo

Ujinga ukosefu wa elimu ndonguzo ya uwepo waccm hadikeo hii,kila

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana. Ila umenena kweli kabisa! We unafanya kazi na kulima au? Halafu elimu yako ni kiwango gani? Pole sana!
 
Mi nadhani ni 'complicated' zaidi ya hii misemo ya "...wanakuzuia kuuza nje ya nchi..." tunayokimbilia kuitumia kila mara kama ndicho kielelezo cha tatizo ambalo kikiondolewa hali ya mkulima itaneemeka hapo hapo!
Mkuu Kalamu1 kipindi fulani hivi nadhani cha Mh. Kikwete unalima mahindi, unauza gunia moja la mahindi kwa 70000/- hadi 100000/- unarudi nyumbani na bati 7 ama 10 kwa hilo gunia na umelima kwa ruzuku ya Serikali kwenye mbolea (25000 - 30000/-) kwa kilo 50. Leo hamna ruzuku ya mbolea, unanunua mbolea 70000/- hadi 100000/- unauza gunia 20000/- unarudi nyumbani umenunua bati 1. Ebu nielimishe wapi kuna matatizo?
 
Sisi tupo hapa anaweza kuja Mchina akafungua kiwanda Rukwa na kuajiri vijana wetu kwa ujira kiduchu. Baada ya miaka mitatu amekua billionaire.
Nikifunga kiwanda cha kusaga sembe songea mfano kuleta dar, ili kuleta unga dar natakiwa niwe na risiti ya efd ambapo kila kiroba tra watakula si chini ya 3000 kww point kuwa unga umeuzwa hata kama bado sijauza, ila nikisafirisha mahindi toka songea kuja dar ntalipia ushuru wa halmashauri 1000 kwa kila mfuko wa kg 100. Kwa semitrailer la viroba 300 ntalipia 300000 kama ushuru tu. LAkini nikisafirisha unga kama naenda kuuza bei ya 17000 ntalazimika ntaingia gharama ya almost 3600000 kabla hata sijajua bei kama itapanda au kushuka.
 
Magu alikua mpigaji hakuna mfano wake,sgr,bwawa la umeme,daraja busisi,kununua madege yasiokua na kazi...yani ufisadi wake ni trilioni za kutosha....uliona wapi miradi inapitishwa na rais bila bunge,wakandarasi katafuta yeye mwenyewe[emoji16][emoji16][emoji16]ccm wote majambazi sugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…