Mkuu 'misasa', tunazunguka tuuu na maneno mengi lakini nadhani sote tunajua tatizo lilipo.
Tatizo lipo huko huko kwenye hiyo serikali unayosema "ina mkono mrefu", lakini haina uwezo wa kuutumia mkono huo mrefu kwa manufaa ya wananchi wake.
Tatizo ni nini? UZEMBE.
Nchi hii hata kutafuta na kuweka takwimu sahihi tu ni shida tupu!
Serikali katika hali ya kawaida kabisa ingeweza kuwa na uwezo wa kujua kiasi cha mazao yanayotegemewa kuzalishwa katika msimu fulani, kabla hata mazao hayajavunwa.
Serikali inao uwezo wa kupata taarifa za masoko duniani kote kabla ya mazao hayajavunwa; na kujua ni nchi gani zitakuwa na uhitaji mkubwa wa mazao hayo, kabla ya msimu wa mazao husika. Hii siyo kazi ya kubahatisha unayoanza kuifanya wakati tayari mazao ya wakulima yakiwa ghalani!
Serikali ina uwezo wa kujenga maghala ya kuhifadhia mazao ya ziada ili kama soko hali siyo nzuri mazao ya wakulima yahifadhiwe, yasiharibike ili soko likipatikana yauzwe.
Serikali ina uwezo kabisa wa kufanya mipango ya kuwakaribisha wawekezaji ili kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa kwa ziada. Mfano. Mahindi siyo chakula cha binaadam pekee. Mahindi yanatoa mafuta ya kula, nasi hapa tunao uhaba mkubwa wa mafuta ya kula, mbona hatutumii mahindi kutuzalishia bidhaa hiyo?
Mahindi yanatengeneza "ethanol' inayoweza kuchanganywa kwenye petroli ili tupunguze gharama za uagizaji wa mafuta, n.k., nk..
Kama kuna malighafi ya kutosha na ya kuaminika (mahindi) itashindikana vipi kuwapata wawekezaji wa kuitumia malighafi hii?
Hebu angalia, kuna wakati ilipigwa kelele nyingi kuhusu zao la mihogo na utengenezaji wa wanga. Kiwanda kikajengwa, nadhani Ruangwa kwa Majaliwa. Wakulima wa mihogo nao sijui ilikuwaje, kiwanda kikasuasua hadi leo hakisikiki
Serikali, kama ulivyosema, ina wajibu wa kuyasimamia mambo haya, si swala tu la kuyapigia kelele kwa msimu na kuyaacha yafe!
TATIZO LIPO SERIKALINI, SIYO KWA WAKULIMA.