Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

Tanzania ya kesho hatujajua itakuwa ya aina gani?

Anyway... Wapinzani pia wamechangia hili kutokea mfano kitendo cha kukubali kushiriki uchaguzi mkuu ilihali uwanja wa kisiasa haupo sawa yaani kukosekana kwa tume huru ilikuwa ni makosa.

Baada ya kushuhudia kilichotokea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana ilikuwa ni kiashiria tosha kwa kitakachotokea mwaka huu ila wapinzani hawakulitilia maanani hili.

Anyway...tuvumilie tu maana wenye nchi yao (wenye madaraka) Provedwametaka iwe hivi.
Mkuu Proved

Wapinzani hawana kosa lolote kushirikiana bila Tume huru.

Wapinzani wakuu wangesusa vijipinzani vitawi vya CCM vingeshiriki,Tena CCM ndio wangeweka Uchaguzi wa Haki na huru kwelikweli ili Kuonesha dunia.

Navyo vijipinzani vitawi vya CCm vingezawadiwa viti viwiliviwili vya majimbo na udiwani.

Mchezo ungeisha.

CCM hawanaga aibu.

Ukishiriki wanakubana,usiposhiriki wanakuwa fare.

Kwa Sasa kwa wapinzani wakuu kushirikiana imesaidia Kuonesha Watanzania wema na Dunia Hali halisi ilivyo hapa Tanzania.

Haya mambo hayajaisha Kuna Mambo makubwa yatatokea.
 
Hivi unajisikiaje wewe mwananchi wa hai, arusha mjini na Moshi mjini, mbeya mjini, mbunge wako kakaa miaka 10+ hamna kitu amefanya alafu unasikia Mwanza, Dar es Salaam, Pwani na mikoa mingine inapaa tu, roho lazma ziume na hayo ndo matokeo
Mimi nasikitika kupoteza muda wangu kwenda kujiandikisha, kupiga kura ila yote kwa yote muda na mwamuzi mzuri.
 
Siyo kwamba naukubali upinzani kwa asilimia mia,ila kukosekana kwa upinzania ni hatari mara mia moja ya kuwepo kwa upinzani,tutegemee upinzania mzito utakaoibuka sasa zaidi ya upinzani wa kususia bunge na kupiga makelele majukwaani,nchi imejiingiza katika mitihani mizito.
Kwa kuwa watu ni mazezeta hawatakuelewa.

Mungu ni mwema sana.
 
Sidhani Kama wewe waweza kuwa mzalendo kumshinda Hayati Mkapa,ama kumshinda Mh Kikwete.
Kabla ya Mkapa kufa alianza kuona atahari za Joni na Kikwete anaziona athari za Joni.
Sidhani Kama Kikwete anafurahi yanayoendelea.
Na ndio maana ya like neno Wastaafu waache kuwashwawashwa.
Uzalendo sio kuchukia Mawazo mbadala.
Wapinzani Ni Watanzania Kama wewe ila wenye mitazamo tofaauti na CCm.
Inawezekana wapinzani wa CCM Ni wazalendo zaidi kuliko CCM.
Asante kwa kusoma post yangu na kuinukuu. Hata hivyo, Sina maoni wala hoja katika katika maelezo uliyotoa.
 
Siongelei wana CCM hapa, nawaongelea upinzani ambao sisi tuliwaamini na kuwatuma lakini wakafika bungeni na kuanza kususia vikao,

Hivi wewe kama baba wa nyumba mkeo akakosea utamsusia na kununa?
Hao waliobaki wanakutetea? hao wapinzani wanatakiwa wakutete dhidi ya nini? kwani wakiondoka bungeni si kuna wabunge wanabaki? au hua linabak jeupe?? waliwah kukutetea hao wanaobaki?

watu 35 vs watu 220+ kwa wabunge wa kuchaguliwa unategemea hao 35 washinde vipi hawa 220 kwa kura za ndio?

what they always do ni kutengeneza awareness , jamii ijue , we tried lakn tumeshindwa, taarifa itakufikia vipi ww ujue utopolo unaofanyika, wanasusia vikao, wewe ukipata taarifa wamesusia vikao si lazima uulize ni kwanini? tayari unapata ujinga uliofanyika..hence wamefanikiwa.
 
This is too much. Hata sisi wana-CCM hatujafurahia. Level ya ubunge ngoma ingeachwa fair at least tukawapata wabunge cream kutoka na upinzani. Ambao kwa ukweli wamekuwa na mchango mkubwa sana sana toka 1992. Leo hii tunaingia kwenye bunge ambalo wabunge wote ni CCM 100%kutoka bara. Labda wa ACT kutoka Pemba kuingia bunge wa JMT, ila napo it depends na kama watakubali au itakuwa kama last time.

Kwa hakika ni uzuni. na wananchi tusishangilie hili. Nchi imeingia katika majaribio makubwa sana. kwa wale slow learners mtaanza kuona madhara yake not even far just 2022.

Nidiriki kusema haijawa njia sahihi na sio afya kwa demokrasia. Mapungufu na wizi ulikuwepo wa kiwango cha juu sana sana. Anyway, tumerudi nyuma hatua 30 katika demokrasia aliyotuachia Baba wa Taifa na Mzee Kikwete.

Hata Mwalimu Nyerere alikuwa anarusu fairness na amekuwa na wabunge wa upinzani before Chama kimoja. Mwinyi naye. Mkapa naye na Kikwete naye. Ila hii ya wabunge wote kutoka bara kuwa CCM... Duuuuh!. kweli tunatofautiana fikra
Kuna wapumbavu wanashangilia sana, hawajui impact ya haya matokeo huko mbeleni, Mungu tusaidie watanzania
 

Tulionya tukapuuzwa, Laana ya Dr. Slaa ni kali
 
Kama Sijakosea kwenye Kumbukumbu zangu yule Dada wa taifa Anaeishi Los Angeles( USA) Alishasema hii hali kitambo sana.
Kuwa Uchaguzi wa 2020 Akuna chama cha Upinzani kitakachopata kiti cha Ubunge.
Kuna viti viwili hadi sasa
 
Upotoshaji Mkubwa,hivi kwa akili ya kawaida,wakati CCM wanawahamasisha wanachama wao kujiandikisha vyama vya upinzani mlikua mkihamasisha watu kudai Tume huru mkaacha ajenda ya kuwatengenezea ushindi.Mlitegemea malaika wawapigie kura_
 
Back
Top Bottom