Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

Mkuu Proved

Wapinzani hawana kosa lolote kushirikiana bila Tume huru.

Wapinzani wakuu wangesusa vijipinzani vitawi vya CCM vingeshiriki,Tena CCM ndio wangeweka Uchaguzi wa Haki na huru kwelikweli ili Kuonesha dunia.

Navyo vijipinzani vitawi vya CCm vingezawadiwa viti viwiliviwili vya majimbo na udiwani.

Mchezo ungeisha.

CCM hawanaga aibu.

Ukishiriki wanakubana,usiposhiriki wanakuwa fare.

Kwa Sasa kwa wapinzani wakuu kushirikiana imesaidia Kuonesha Watanzania wema na Dunia Hali halisi ilivyo hapa Tanzania.

Haya mambo hayajaisha Kuna Mambo makubwa yatatokea.
 
Hivi unajisikiaje wewe mwananchi wa hai, arusha mjini na Moshi mjini, mbeya mjini, mbunge wako kakaa miaka 10+ hamna kitu amefanya alafu unasikia Mwanza, Dar es Salaam, Pwani na mikoa mingine inapaa tu, roho lazma ziume na hayo ndo matokeo
Mimi nasikitika kupoteza muda wangu kwenda kujiandikisha, kupiga kura ila yote kwa yote muda na mwamuzi mzuri.
 
Kwa kuwa watu ni mazezeta hawatakuelewa.

Mungu ni mwema sana.
 
Asante kwa kusoma post yangu na kuinukuu. Hata hivyo, Sina maoni wala hoja katika katika maelezo uliyotoa.
 
Siongelei wana CCM hapa, nawaongelea upinzani ambao sisi tuliwaamini na kuwatuma lakini wakafika bungeni na kuanza kususia vikao,

Hivi wewe kama baba wa nyumba mkeo akakosea utamsusia na kununa?
Hao waliobaki wanakutetea? hao wapinzani wanatakiwa wakutete dhidi ya nini? kwani wakiondoka bungeni si kuna wabunge wanabaki? au hua linabak jeupe?? waliwah kukutetea hao wanaobaki?

watu 35 vs watu 220+ kwa wabunge wa kuchaguliwa unategemea hao 35 washinde vipi hawa 220 kwa kura za ndio?

what they always do ni kutengeneza awareness , jamii ijue , we tried lakn tumeshindwa, taarifa itakufikia vipi ww ujue utopolo unaofanyika, wanasusia vikao, wewe ukipata taarifa wamesusia vikao si lazima uulize ni kwanini? tayari unapata ujinga uliofanyika..hence wamefanikiwa.
 
Kuna wapumbavu wanashangilia sana, hawajui impact ya haya matokeo huko mbeleni, Mungu tusaidie watanzania
 

Tulionya tukapuuzwa, Laana ya Dr. Slaa ni kali
 
Kama Sijakosea kwenye Kumbukumbu zangu yule Dada wa taifa Anaeishi Los Angeles( USA) Alishasema hii hali kitambo sana.
Kuwa Uchaguzi wa 2020 Akuna chama cha Upinzani kitakachopata kiti cha Ubunge.
Kuna viti viwili hadi sasa
 
Upotoshaji Mkubwa,hivi kwa akili ya kawaida,wakati CCM wanawahamasisha wanachama wao kujiandikisha vyama vya upinzani mlikua mkihamasisha watu kudai Tume huru mkaacha ajenda ya kuwatengenezea ushindi.Mlitegemea malaika wawapigie kura_
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…