Nchi imejaa ushabiki wa ajabu, sijui kama ipo siku tutasimama kama Taifa

Nchi imejaa ushabiki wa ajabu, sijui kama ipo siku tutasimama kama Taifa

IMG-20240322-WA0002.jpg

Waziri Ndumbaro akiwapatanisha GENTAMYCINE pamoja na Chizi Maarifa ili wawe wazalendo kwa nchi yao.
 
Salaam,

Kuna sintofahamu imetokea baada ya waziri Damas Ndumbalo kutoa maelekezo kwa mashabiki wa sokq nchini ya kuwa inabidi Watanzania woote tusimame kwa ajiri ya nchi, na upinzani wetu wa simba na yangu tuuweke pembeni kwanza, mhimu ni simba na yangu tuziunge mkono kama taifa na kwa masirahi ya nchi.

Kilichotokea ametukanwa matusi yoote, na amedharirishwa utafikili hilo amelifanya kwa masirahi yake binafsi na familia yake, au kafanya kwa masirahi ya CCM. mie ninajiuliza, ni lipi hasa kosa la Ndumbaro?

Mbona nchi nyingine huwa tuna ona jinsi walivyo wazalendo? Ninasikitika huu mpasuko na mgawanyiko wa taifa letu.
Kwa upande wangu naona kulikuwa na njia nyingi za kuhamasisha uzalendo ila sio kwa namna aliotumia, kiufupi ni halali akosolewe
 
Hayati RAIS Mwinyi alihudhuria mechi ya Simba na Stella Abijan , kabla ya hapo alisisitiza sana uzaelendo lakini wakati Stella wanapata goli la pili mashabiki wa YANGA walianza kuimba na kuzunguka uwanja mzima wakisema Uzalendo umewashinda.
Yanga ama mashabiki wa Yanga wamekuwa vinara sana wa kukodisha Coasta na kwenda kupokea timu pinzani zinapocheza na Simba.
Hersi siku ya mechi ya Simba na KAIZER chief alivaa jezi ya Kaizer Chief.
Juzi Jwaneng walipokuja kucheza walifikia Avic Town mahali ambapo ni kambi ya Yanga.

Waziri anataka Uzalendo gani? Wewe mleta mada una timu unaishaibikia ambayo ni ya Uiengereza au Hispania lini waziri amekuzuia? Wenzetu Ulaya kila shabiki wa mpira ni shabiki wa timu inayotokea eneo analoishi, je wewe unashabikia timu ya mkoani kwenu?

Uzalendo ni timu ya Taifa si Yanga au Simba, kama mnataka uzalendo anzani sasa kuweka mikakati kila shabiki aingie uwanjani siku timu yake inacheza tu. Lakini utakuta kila Simba ikicheza mashabiki wa YANGA wamejaa uwanjani, kufanya nini? Kila mtu ashinde mechi zake.
Hata msemaji wa hayo yenyekuleta mjadala ashinde mechi zake kivyake🏃‍➡️🏃‍➡️🏃‍➡️
 
Back
Top Bottom