Pagan Amum
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 1,932
- 4,403
Zikiwa zimebaki siku 3 kabla hatujaingia tarehe 28.10.2020 siku ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu Tanzania, nadiriki kusema kuwa nchi naona inamtaka Lisu. Nimezunguka Mikoa 25 ya Bara na 3 ya Zanzibar, nimepita kila pembe ya nchi. Nimezunguka vijijini sana na kila kona ya nchi hii kwa shughuli za kikazi katika NGO aiseeee sijui nini kitokee ila nimeshuhudia kwa macho yangu na kuona namna Lisu anavyokubalika sana sana.
Ambacho sikuamini ni mwamko walionao vijijini ni mkubwa kuliko hata wa majiji. Vijijini wanasema kwa hii njaa ya miaka 5 hawawezi tena kuipa serikali hii kura. Jana nilivyokuwa narudi Dar es Salaam, nilipita takriban mikoa 7 kutoka kanda ya ziwa nimeshuhudia namna Mawakala wa upinzani walivyojipanga na kupeana semina wenyewe kwa wenyewe.
Bahati mbaya zikwenda kukusanya data za kisaisa ila kwa haya nilioyaona katika hiyo Mikoa 28 sioni namna Tundu Lisu akashindwa huu uchaguzi. Watu wamechoka, watu wana njaa, watu hawana fedha, watu wamekosa matumaini. Tena ukiwauliza maswali wanakujibu waziwazi kuwa kwa mbunge huyo sawa tutampa wa CCM ila suala la Urais Hapana tunampa "Mbeba Maono"