Mwanamke ameumbwa kuwa msaidizi kwa kufanya mambo madogomadogo. Kiherehere chetu tumeamua kuwapa majukumu makubwa na wanaume ndio tumegeuka wasaidizi kwa msukumo wa kile tunachokiita usawa wa kijinsia.
Tusichokizingatia ni kuwa wanaotushawishi huo usawa wao wana mipaka, kuna maeneo hawawezi kujichanganya kujaza akina mama, wakati sisi kila sehemu tunawajaza kwa kasi. Eti kwa sababu tuna rais mwanamke basi utakuta kila sehemu kuanzia kwenye mihimili ya nchi, huko ccm n.k wanawake wanapewa kipaumbele tu hata kama uwezo wao ni mdogo kwa lengo kuu linalowekwa wazi bila hata soni kuwa ni kumfurahisha namba 1!